Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb), tarehe 22 Novemba, 2026, amemtembelea na kumjulia hali Mkuu wa kwanza wa Majeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jenerali Mirisho Sam Hagai Sarakikya (Mstaafu), nyumbani kwake Tengeru, mkoani Arusha. Katika ziara hiyo, Waziri wa Ulinzi na JKT, Dkt Rhimo Nyansaho amepata fursa ya kufanya mazungumzo na Jenerali Sarakikya, ikiwa ni sehemu ya kuendeleza mawasiliano na ukaribu na kiongozi huyo aliyewahi kuliongoza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
Ikumbukwe kuwa hii si mara ya kwanza kwa Waziri wa Ulinzi na JKT kumtembelea Jenerali Sarakikya, jambo linaloonesha mwendelezo wa mawasiliano na kutembeleana kati yao. Ziara hiyo pia imetoa fursa ya Waziri kupata nafasi ya kuzungumza na kiongozi huyo mstaafu na kumtambua kwa nafasi yake ya kihistoria katika uongozi wa JWTZ.






No comments:
Post a Comment