#GoodNews single mpya ya Joh Makini feat AKA kutambulishwa leo kwenye MTV Base! - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, November 10, 2015

#GoodNews single mpya ya Joh Makini feat AKA kutambulishwa leo kwenye MTV Base!



Ni time ya kuzipata #Goodnews za Bongo Flevani… baada ya Nikki wa Pili kuitambulisha single yake mpya ‘Baba Swalehe’ Ijumaa iliyopita, sasa ni zamu ya kichwa kingine kutoka WEUSI kuwasogezea mashabiki wake wa Tanzania na Africa flava mpya ya muziki wa Bongo Flava.
Miezi kadhaa iliyopita Joh Makini alidondoka pande za South Africa ambako alikutana na mkali mwengine wa muziki wa HipHop pande hizo, AKA na wawili hao wakaingia studio na kutengeneza wimbo ambao leo tarehe 10 November 2015 single hiyo itatambulishwa kwa mara ya kwanza kwenye MTV Base kama #SpankingNew!
JOHAKA3
Wimbo mpya wa Joh Makini unaitwa ‘Don’t Bother’ na unatambulishwa leo kwa mara ya kwanza kupitia kituo cha MTV Base saa 12 jioni (1800hrs EAT) saa za Africa Mashariki… Mtayarishaji wa ngoma hii mpya ni mtu wetu Nahreel kutoka The Industry huku Video Director wa wimbo huo akiwa Justin Campos wa Gorilla Films kutoka South Africa.
JOHAKA2

No comments:

Post a Comment