Mwanasoka wa zamani wa timu ya taifa ya Rwanda na klabu ya Rayon Sports ya Rwanda Hamad Ndikumana amerudi tena katika headlines za soka November 20, Ndikumana ambaye ni mume wa muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya ametemwa na klabu yake ya Stand United baada ya kocha wa timu hiyo mfaransa Patrick Liewig kutohitaji huduma yake.
Ndikumana ambaye alikuwa na klabu ya Stand United ya Shinyanga kwa kipindi cha miezi minne ametemwa rasmi na klabu hiyo, hivyo kwa sasa ni mchezaji huru, awali Ndikumana aliwahi kugoma kuichezea klabu hiyo baada ya kutomaliziwa malipo yake lakini msemaji wa Stand United ya Shinyanga Deokaji Makomba amethibitisha kuwa moja kati ya sababu zilizofanya wamuache staa huyo ni umri wake kuwa mkubwa.
“Kocha
amesema hatomuhitaji tena katika kikosi chake sababu kubwa ilitajwa na
mwalimu ya kumuacha Hamad Ndikumana ni kuwa na umri mkubwa hivyo mwalimu
kaona aachane nae kwani itakuwa ngumu kuendelea nae, Hamad Ndikumana
hatupo nae tena na tayari ameshakamilishiwa haki zake” >>> Deokaji Makomba
Ndikumana
ambaye amewahi kutamba na vilabu kadhaa anatajwa kuwa na umri wa miaka
37, umri ambao ni mkubwa kisoka, kama utakuwa unakumbuka vizuri Ndikumana ndio jamaa ambaye alimuoa mrembo kutoka kiwanda cha filamu za Kibongo Irene Uwoya na kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume anaitwa Krish.
No comments:
Post a Comment