Moja kati ya michezo inayotajwa kuvuta hisia za mashabiki wengi wa soka duniani ni mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya FC Barcelona zote za Hispania, mchezo huu ambao unaitwa El Clasico ni mchezo ambao tunaweza kuufananisha na upinzani wa Simba na Yanga. Kabla ya mchezo wao wa Jumamosi ya November 21 mtu wangu naomba nikusogezee mambo matano ya kufahamu kuelekea mchezo huo.
1- Ni mchezo unaowakutanisha wachezaji wenye rekodi ya kipekee Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, wote wanarekodi ya kuwa wachezaji pekee kuwa nominated katika kuwania tuzo ya Ballon d’Or kwa miaka nane mfululizo, rekodi ambayo hakuna wachezaji waliowahi kuiweka, Messi ametwaa tuzo hiyo mara 4 na Ronaldo mara 3.
2- Hii ndio itakuwa mechi ya El Clasico ya kwanza toka mwaka 1999 kuchezwa bila uwepo wa golikipa namba moja wa zamani wa Real Madrid Iker Casillas aliyetimkia FC Porto ya Ureno na kukosekana kwa kiungo wa zamani wa FC Barcelona Xavi Hernandez.
3- Klabu ya Real Madrid ndio inaongoza kuifunga FC Barcelona mara nyingi, imeifunga jumla ya mechi 92 wakati FC Barcelona wameifunga Real Madrid mara 89.
4- Tayari Lionel Messi aliyekuwa majeruhi kwa takribani wiki nane anatajwa kuanza mazoezi na huenda akawepo katika mchezo wa El Clasico utakaochezwa November 21 kama madaktari wake watathibitisha kuwa yuko sawa kurejea uwanjani. Ila November 17 Messi alionesha kiatu chake kipya atakachochezea mechi ya El Clasico.
5- Messi na Ronaldo ndio wachezaji wenye rekodi ya kipekee, kwani tofauti ya umri wao ni sawa na tofauti wa umri wa watoto wao. Ronaldo ni mkubwa kwa Messi yaani amemzidi Messi siku 869, ambapo ni utofauti wa mtoto wa Messi ambaye anaitwa na Thiago na utofauti wa mtoto wa Ronaldo anayeitwa Cristiano Ronaldo Junior ambapo yeye pia ni mkubwa kwa mtoto wa Messi kwa siku 869.
No comments:
Post a Comment