November 18 uongozi wa klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba ulitoa Press release kuhusu kiungo wa kimataifa wa Uganda anayekipiga katika klabu ya Azam FC Brian Majwega kuomba kujiunga kufanya mazoezi na Simba wakati huu wa Ligi, kitu ambacho kimeshangaza wengi kwa nini aombe kufanya mazoezi na Simba wakati ni mchezaji wa Azam FC na klabu ya Azam FC inaanza mazoezi Jumatatu ya November 23.
millardayo.com ilipata nafasi ya kumtafuta afisa habari wa Azam FC Jafari Iddi Maganga na kuomba kufahamu kuhusu maamuzi hayo ya Majwega au wamemtoa kwa mkopo katika klabu ya Simba na hawajataka kuweka wazi, mkataba wake umemalizika? kuna tatizo gani kati ya Majwega na Azam FC.
”
Majwega hatujampeleka klabu yoyote kwa mkopo ila ametoroka kambini na
kwenda kwao Uganda lakini Uganda hawezi kucheza klabu yoyote kwa sababu
ana mkataba na Azam FC hivyo hawezi kucheza klabu yoyote, kuhusu
kufanya mazoezi na Simba hatuwezi kuzungumzia hatujui wameongea nini ila
licha ya kutoroka Azam FC haikumchukulia hatu yoyote ila kwa
anachokifanya sasa anahitaji apate adhabu” >>> Jafari Iddi
No comments:
Post a Comment