Rais Barack Obama
anakaribia kumaliza muhula wake wa pili kuiongoza Marekani tangu mwaka
2008, lakini kuna tabia yake aliyokuwa nayo muda mrefu ya kuvuta sigara…
alipoingia White House aliendelea kuvuta?
Obama alihojiwa na kwenye sentensi za kwanza kajibu hivi >>> “Sijavuta
sigara hata moja ndani ya miaka mitano tangu nimeingia Ikulu… Niliahidi
kwamba Muswada wa Sheria mpya ya Afya ukipita (2010) sivuti tena
sigara, na kweli imetimia“.
Obama
anasema alijaribu mara kadhaa kuachana na sigara mwaka 2008 wakati wa
Kampeni za Urais lakini ilishindikana, kuna wakati alijikuta akijibana
zake kona na kuvuta tena na tena !!
Unajua kingine alichojibu Rais Obama kuhusu kuacha kuvuta sigara >>> ‘Namuogopa mke wangu’… Michelle kumbe nae hakuipenda tabia ya uvutaji sigara ya Obama iendelee !!
Achana na hayo, swali jingine la kizushi kwa Obama… akiwa zake ‘out’ na Michelle wake wanakula raha, simu ya nani anaweza kupokea ikiita? >>> “Mmmmh…
labda ya Malia, Sasha (watoto wake) na mama mkwe.. nyingine ya mshauri
wangu wa usalama Susan Rice, na Katibu Mkuu Kiongozi, Denis McDonough” >>> Barack Obama.
Basi hayo ndio majibu ya Rais Obama, kuna kitu hukutegemea kwamba angekijibu kwenye hayo?
No comments:
Post a Comment