
Real Madrid na Barcelona zitaumana kwenye mchezo wao wa ligi maarufu
kama El Clasico utakaochezwa kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu Jumamosi
ya November 21, katika historia ya mchezo huo Real Madrid maarufu kama
Los Blncos wao ndio wanaongoza kushinda idadi ya mechi nyingi wakiwa
wameshinda michezo 92 wakati Barelona wao wakiwa wameshinda mechi 89.
Kabla hujakaa chini kuangalia mchezo huo siku ya Jumamosi,
inawezekana kuna baadhidi ya vitu ambavyo huvifahamu kuhusu mchezo huo
mkubwa kwenye historia ya soka.
- Ushindi mkubwa kwenyehistoria ya mchezo wa El Clasico
Real Madrid 11-1 Barcelona (13 June 1943)

Kwenye
msimu wa mwaka 1943, Barcelona iliifunga Real Madrid magoli 3-0
nyumbani kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya kombe la Copa del
Rey, lakini kikosi cha Real Madrid kilionesha kiwango kizuri kuwahi
kutokea kwenye mchezo wa soka na kufanikiwa kuifunga Barcelona bao 11-1
kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu kwenye mchezo wa marudiano na kutinga
hatua ya fainali ya kombe hilo.
- Kipindi kirefu bila kupoteza mchezo wa El Clasico
Barcelona: Mechi 13 (1 November 1917- 3 June 1928)

Barcelona
iliweza kucheza kwa miaka 11 bila kupoteza mchezo dhidi ya Real Madrid
kwenye mashindano yote kuanzia November 1, 1917 hadi June 3, 1928,
watoto wa Catalan pia wanashikilia rekodi ya kukaa muda mrefu zaidi bila
kufungwa kwenye mchezo wa El Clasico kwenye ligi (La Liga) ikiwa
hawajapoteza michezo saba, kuanzia December 2008 hadi December 2011
wakifanikiwa kushinda michezo sita kati ya saba.
- Mfungaji bora wa muda wote kwenye El Clasico
Lionel Messi: Magoli 21

Lionel
Messi ndiye mcheaji anayeongoza kutupia kambani kwenye mechi ya El
Clasico akiwa kafunga magoli 21 kwenye michezo 30 aliyocheza. Magoli 14
kwenye mechi za ligi (anafungana na Di Stefano), amefunga magoli matano
kwenye michuano ya Super Cup na magoli mawili kwenye UEFA Champions
League.
- Rekodi ya Kufunga mfululizo kwenye El Clasico

Cristiano Ronaldo: Mechi 6
Cristiano Ronaldo anashikilia rekodi ya mchezaji ambaye amefunga
mfululizo kwenye mechi za El Clasio akiwa amefunga magoli 7 kwenye mechi
6 zilizopita tangu 2011-2012 Copa del Rey (mechi ya raundi ya kwanza)
hadi 2012-13 mechi ya La Liga.
- Nidhamu mbovu kwenye mechi za El Clasico
Fernando Hierro: Kadi 19

Mchezaji
wa zamani na nahodha wa Real Madrid Fernando Hierro anaonekana kama
mchezaji mwenye nidhambu mbovu kuwahi kutokea kwenye historia ya mechi
za El Clasico akiwa amepewa jumla ya kadi 19 kwenye historia ya mchezo
huo. Kati ya kadi hizo, 18 ni za njano huku moja ikiwa ni nyekundu.
Ramosi anaongoza kupewa kadi kwa wachezaji wa sasa, ameshaoneshwa kadi 16 (kadi 14 za njano na nyekundu mbili.
No comments:
Post a Comment