Klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Jumapili ya November 8 itacheza mchezo wake wa pili wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na USM Alger ya Algeria mjini Lubumbashi. TP Mazembe watacheza mchezo huo wa pili wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kuifunga USM Alger katika mchezo wa kwanza uliyochezwa Algeria kwa jumla ya goli 2-1.
Kuelekea mchezo huo klabu ya TP Mazembe wamefanya kitu tofauti kidogo na timu nyingi za Afrika ambazo tumezoea kuona zikihusishwa na imani za kishirikina, hususani zikiwa zinaelekea katika mechi ngumu kama hiyo, TP Mazembe walikusanyika na mashabiki wao na mmiliki wa klabu hiyo Moise Katumbi Chapwe na kwenda pamoja kufanya ibada kanisani ili kuomba mungu wapate matokeo mazuri.
Kitendo walichofanya TP Mazembe
inaripotiwa kuwa huwa ni kawaida yao kufanya ibada hususani wakiwa
wanaelekea katika mchezo mgumu, hii inashangaza kidogo kwani kwa
kumbukumbu za karibuni haijawahi kufanywa na klabu za Tanzania zaidi ya kusadikiwa kufanya ushirikina katika mechi zao.
No comments:
Post a Comment