WAKALA WA GARBA ‘AWAGONGA’ YANGA SC SH MILIONI 200 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, December 12, 2015

WAKALA WA GARBA ‘AWAGONGA’ YANGA SC SH MILIONI 200



WAKALA wa kiungo wa kimataifa wa Niger, Issoufou Boubacar Garba (pichani juu) amewaambia Yanga SC watoe dola za Kimarekani 100,000 (zaidi ya Sh. Milioni 200) kama wanataka huduma ya winga huyo.

Kamati hiyo ililazimika kufanya kikao kujadili suala la mchezaji hiyo baada ya kupata salamu nzuri za awali kwamba Garba anafanya vizuri mazoezini Tanga.
Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji yuko nje ya nchi, lakini atakaporudi kuanzia Jumatatu atahitaji kupewa pendekezo kamili juu ya usajili wa mchezaji huyo.
 
Tayari dalili zinaonyesha kocha Hans van der Pluijm amevutiwa na Garba baada ya mazoezi ya siku mbili mjini Tanga tangu awasili kwa majaribio.
Yanga SC iliyoweka kambi katika hoteli ya Kwetu mjini Tanga kujiandaa na mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara juzi imefanya mazoezi Uwanja wa sekondari ya Galanosi, wakati jana asubuhi ilikuwa Mkwakwani.
Na Garba ameshiriki kikamilifu mazoezi yote hayo kiasi cha kumvutia uwanjani kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm.
Pluijm ambaye anatakiwa kuamua kuhusu mchezaji huyo wa zamani wa Club Africain na
ES Hammam-Sousse za Tunisia kabla ya kufungwa pazi la dirisha dogo la usajili Desemba 15, alionekana kufurahia kila mchezaji huyo alipokuwa na mpira.
Na jana asubuhi katika mazoezi ya kupiga mikwaju ya penalti, Pluijm alifurahia Garba alipofunga kiufundi. 
Garba aliyezaliwa mji wa Niamey, mwenye urefu wa futi 5 na inchi 6, kisoka alianzia klabu ya AS FAN ya kwao mwaka 2010, kabla ya kuhamia Thailand ambako alichezea klabu za Muangthong United mwaka 2011 na Phuket.
Mwaka 2012 alitua Club Africain ya Tunisia ambako hakucheza mechi hadi anahamishiwa 
ES Hammam-Sousse ambako pia hakucheza.
Wasifu wake unaonyesha tangu ameondoka ES Hammam-Sousse hajapata timu nyingine, lakini uongozi wa Yanga SC umejiridhisha anachezea klabu bingwa ya kwao, AS Douanes.

No comments:

Post a Comment