Kijana Baraka Elias Mashauri mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa Musoma mkoani Mara ameshindwa kupata matibabu katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) kutokana na urefu wake usio wa kawaida.
Baraka
anayesumbuliwa na tatizo ya nyonga ana kimo kirefu cha zaidi ya futi 7
na hii kufanya kushindwa kupatiwa matibabu kufuatia vifaa katika
taasisi hiyo ikiwemo mashine za X- ray vitanda vya kufanyia upasuaji
kuwa vifupi ukilinganisha na urefu wake.
Tatizo
hilo la nyonga linalomsumbua Baraka limemfanya ashindwe kutembea na
kulazimika kutumia magongo ambayo anasema yanamtesa kutokana na urefu
alionao.
Akizingumzia
jinsi watu wanavyomshangaa kutokana na urefu wake alisema kuwa kwake
anaona fahari kwani ni maisha ambayo ameyazoea kila anapokwenda. Amesema
kuwa hiyo haimpi shinda kwani anajua wanamshangaa kutokana na urefu
wake kitu ambacho si kibaya.
Kuhusu
ugonjwa unaomsumbua na baada ya kushindikana kupatiwa matibabu nchini,
Baraka ameomba wasamaria wema waweze kumsaida ili apatiwe matibabu nje
ya nchi ili arudie kwenye hali yake ya kawaida kwani magongo
anayotumia kutembelea yanamtesa.
No comments:
Post a Comment