Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla, akiwa ameongzana na timu ya Serikali yenye wataalamu na wanausalama wameendesha operesheni kali ya kusaka viroba feki na pombe nyingine haramu katika maeneo ya Jiji la Dar es Salaam na kufanikiwa kukama shehena kubwa ya bidhaa hizo feki na haramu kwenye maeneo hayo.
Katika operesheni hiyo, pia wamefanikiwa kukibaini kiwanda bubu kinachotengeneza kinywaji aina ya konyagi na Smirnoff feki maeneo ya Sinza Jijini Dar es Salaam.
Kiwanda
hicho kinatengeneza vinywaji hivyo kwa kutumia ‘spirit’ ambayo
inachanganywa na ‘gongo’; spirit, gongo, chupa tupu na zilizojazwa,
vizibo, vifungashio vimekamatwa.
Kwa
hatua hiyo Jeshi la Polisi linawashikilia watu wawili ambao inasemekana
wanafanya kazi pamoja na bwana Yusuf Abdul Kalambo, ambaye anatafutwa
na polisi mpaka sasa kwa tuhuma za kuendesha shughuli hizo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa ameshika vifuniko vya bidhaa za pombe feki katika moja ya kiwanda bubu cha kutengeneza pombe hizo aina ya Konyagi. katika zoezi hilo eneo la Sinza
No comments:
Post a Comment