Serikali imeagiza idara ya uhamiaji nchini kufanya uhakiki upya wa vibali vya wahamiaji wote walioko nchini na kwa wale ambao hawana sifa zinazostahili warudishwe kwenye nchi zao kwakuwa wanaishi nchini kinyume na sheria za nchi zinavyoelekeza.
Agizo
hilo limetolewa jana na waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mhe. Mwigulu
Nchemba alipokutana na viongozi wa idara ya uhamiaji nchini kwaajili ya
kujadili na kutatua kero mbalimbali katika idara hiyo.
Kwa
upande wa mifumo ya utoaji vibali Mhe. Mwigulu ameiagiza idara hiyo
iunde tume maalum ya kujadili nakuangalia namna ya kuweka mifumo maalum
ya kutoa vibali vya uraia kwa urahisi ili kupunguza malalamiko na
ufisadi ambao kama hautatatuliwa mapema utasababisha hasara kwa taifa.
Aidha
aliwaagiza watawala katika idara hiyo kutenda haki kwa watumishi wake
na watanzania kwa ujumla sambamba na kuwalipa madeni yao watumishi wapya
walioajiriwa na idara ya uamiaji nchini.
No comments:
Post a Comment