Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa iliyotolewa katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusu ombi la kurekebisha bei za umeme kwa mwaka 2017.
Ombi la mabadiliko ya bei za umeme liliwasilishwa EWURA kulingana na agizo la kubadilisha bei za umeme la mwaka 2016 lililoanza kutumika tarehe 1 April 2016. Ifahamike kuwa bei za umeme (Electricity Tariffs) zinazotumika zilitolewa zitumike mpaka tarehe 31/12/2016, hivyo itakapofika Januari 2017, inatakiwa bei mpya za umeme (NewElectricity tariff) kutolewa kwa mujibu washeria.
Hivyo
TANESCO ilitakiwa kufanya tathmini ya gharama za uzalishaji ,
usafirishaji na usambazaji umeme na kupeleka mapendekezo hayo kwenye
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji, (EWURA), ili kupitiwa
na kufanyiwa taftishi, (kupata maoni ya wadau), ikiwa ni pamoja na
Baraza la Ushauri la Serikali . Hivyo basi ikiwa bei za umeme
zitapanda au kutopanda, hiyo itategemea na mapitio ya tathmini ya
gharama za kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme tulizowasilisha
EWURA.
TANESCO
haiwezi kuamua yenyewe kupandisha au kutopandisha bei za umeme.
Kwamujibu wa sheria, EWURA inapaswa ifanye mapitio ya bei za umeme kwa
kila robo mwaka (Periodic Tariff Adjustment).
Tunapenda
Umma ufahamu kuwa kupanda au kushuka kwa gharama za umeme ni suala la
kisheria na nijambo la kawaida kwani bei ya umeme imeshawahi kushuka
katika vipindi tofauti kwa mfano Mwaka 2015 (roboya kwanza yamwaka) bei
ilishuka kwa asilimia 2.5. Vivyo hivyo Mwezi Aprili mwaka 2016 pia
gharama za umeme zilishuka kwa asilimia 1.6
IMETOLEWA NA:
Mhandisi FELCHESMI MRAMBA
Mkurugenzi Mtendaji
Shirika La Umeme Tanzania, (TANESCO)
No comments:
Post a Comment