Mwanasiasa mkongwe na waziri wa zamani wa Serikali ya awamu ya kwanza hadi ya nne, Joseph Mungai, amefariki dunia.
Mungai aliyezaliwa Oktoba 24,1943 alifariki dunia Dar es Saalam jana baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Akisimulia
mazingira ya kifo cha baba yake, mtoto wa marehemu, William Mungai,
jana alisema baba yake alifariki dunia wakati akipelekwa katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu.
Alisema
kabla ya kifo hicho baba yake alianza kulalamika kuumwa na tumbo na
kutapika ambako alipelekwa katika hospitali moja ambayo hakutaka
kuitaja.
Alisema
baada ya kufikishwa hospitalini hapo, hali yake ilizidi kubadilika na
kuwa mbaya zaidi na hivyo wakaamua kumkimbiza Muhimbili kwa matibabu
zaidi.
“Ni
kweli baba amefariki dunia saa 10 jioni leo (jana) wakati tukimpeleka
Muhimbili baada ya kulalamika kuumwa na tumbo. Hivi tunavyoongea, ndiyo
tunatoka Muhimbili ila taarifa zaidi tutawapatia baada ya kikao cha
ndugu,” alisema William kwa kifupi.
Ingawa
William hakutaka kuzungumzia kifo hicho kwa undani, taarifa
zilizopatikana na ambazo hazijathibitishwa, zinasema kiongozi huyo
alikunywa kinywaji katika hoteli moja maarufu ya Dar es Salaam.
Watu
walio karibu na familia ya Mungai mameeleza kuwa, jana mchana Mungai
alikuwa katika hoteli hiyo iliyopo Msasani akipata kinywaji kwa kuwa
alikuwa na mazoea ya kufika mahali hapo.
“Mzee jana alikuwa katika hoteli hiyo
akiendelea na kinywaji akipendacho cha whisky. Inasemekana baada ya
kutoka hotelini hapo na kurudi nyumbani kwake, alianza kutapika huku
akilalamika kusikia maumivu makali ya tumbo.
“Vijana
wake walimpeleka hospitali ya karibu, lakini hali ilizidi kuwa mbaya
ndipo familia iliamua kumkimbiza Muhimbili ambako aliaga dunia,” alisema mtoa taarifa huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake.
Mungai aliwahi kuwa Mbunge wa Mufindi kupitia CCM kwa miaka 35.
Pia
amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini enzi za utawala wa
Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na pia katika awamu za
pili, tatu na nne.
Baadhi
ya nyadhifa alizowahi kushika kwa nyakati tofauti ni uwaziri wa
iliyokuwa Wizara ya Elimu na Utamaduni, Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya
Mifugo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment