WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku 18 kwa Mkandarasi wa umeme kwenye
kiwanda cha Kiluwa Steel Group awe amemaliza kazi ya kuweka ume mkubwa
ili kiwanda hicho kianze kazi.
Ametoa
agizo hilo jana (Jumamosi, Novemba 19, 2016) wakati akizungumza na
wananchi na viongozi mbalimbali wa Serikali na wa Mkoa wa Pwani
waliofika kiwandani hapo eneo la Mlandizi wakati akikagua utekelezaji wa
maagizo aliyoyatoa Julai 12, mwaka huu alipozuru kiwanda kwa mara ya
kwanza.
“Nilipokuwa
hapa mara ya kwanza niliagiza itengenezwe njia ya reli kutoka njia
panda ya reli ya kati, lakini pia niliagiwa uwekwe umeme wa msongo
mkubwa ili kiwanda kiweze kuanza uzalishaji mapema mwakani. Nimefarijika
kukuta maagizo haya yametekelezwa kwa kiasi kikubwa isipokuwa hili la
umeme,” alisema.
“Mkandarasi
ameomba siku 14, nimempa hadi tarehe 7 Desemba ahakikishe umeme
unafanya kazi kwa kiwango kinachotakiwa. Sasa hivi wameanza test lakini
muda ili transforma iweze kuhimili mzigo mkubwa… hili ni suala la
kitaalamu kwa hiyo tuwape muda.”
Waziri
Mkuu pia alisema amefarijika kusikia kwa orodha ya watu wanaodai fidia
sababu ya kuoisha njia ya reli ijengwe, imeshawasilishwa kwa Mkuu wa
Mkoa na mwenye kiwanda yuko tayari kuwalipa maa taratibu
zitakapokamilika.
Mapema,
akiwasilisha taarifa fupi, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Eng. Evarist Ndikilo
alisema haelewi ni kwa nini mkandarasi huyo anazidi kuomba siku 14 ili
kukamilisha wakati aliahidi kuwa 14 za awali zingetosha kukamilisha kazi
hiyo.
Kuhusu
fidia kwa wananchi na Halmashauri ya Wilaya hiyo, Mkuu huyo wa Mkoa
alisema wananchi waliopisha njia wanadai fidia ya sh. milioni 95.76 na
Halmashauri inadai sh. milioni 307.26 na kwamba jumla yote inafikia sh.
milioni 403.
Alipopewa
nafasi na Mkuu wa Mkoa huo ajieleze mbele ya Waziri Mkuu, Mkurugenzi
Mkuu wa kampuni ya Dekan Group Ltd, Eng. Desderius Luhaga ambaye amepewa
kazi ya kuweka umeme na transforma Mlandizi alisema anahitaji apewe
siku 14 ili aweze kukamilisha kazi hiyo.
“Kazi
kubwa ya umeme tumeshaifanya na hii ni ya umeme wa msongo wa kilovoti
132, na tumeanza kutest umeme katika baadhi ya mitambo hapa kiwandani,
lakini tunahitaji siku karibu tano ili transforma ipoe tangu
tulipoifunga ndipo iweze kupokea mzigo mkubwa. Kisha tutaanza
kuunganisha katika maeneo mengine madogo madogo humu ndani,” alisema.
Katika hatua nyingine,
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Bw. Masanja
Kadogosa alisema shirika hilo limetumia sh. milioni 863 kukamilisha
ujenzi wa reli ya km.5 kutoka njia panda hadi kwenye kiwanda hicho
ambapo kati ya hizo km.1.5 zimo ndani ya kiwanda.
Alisema hadi sasa wameshaweka njia nne za reli, moja ikiwa ni mahsusi kwa ajili ya kubeba makaa ya mawe.
“Tulilazimika
pia kujenga culvert katika eneo moja kwa sababu pailikuwa na shimo
kubwa. Tumetumia fedha kidogo kwa sababu tumetumia mafundi wetu badala
ya wakandarasi,” aliongeza.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa Kiluwa Steel Group, Bw. Mohammed Kiluwa alimweleza
Waziri Mkuu kuwa anatarajia kuanza uzalishaji Januari, mwakani na kwamba
ataajiri wafanyakazi wapatao 200.
“Tunataraji
kuanza uzalishaji Janruari, mwakani na uzalishaji utakuwa tani 2,000
kwa siku. Ila tumekubaliana na wawekezaji wenzangu tuweke pia viwanda
vingine vitatu kwa sababu kutakuwa na umeme wa kutosha.”
“Tunatarajia
kufungua viwanda vine vya kutengeneza gypsum powder, pikipiki, nguzo na
vifaa vya kufungia nyaya za umeme mkubwa pamoja na tissue. Tuna eneo
lingine Mkuranga lakini kule hakuna umeme, kwa hiyo tumepanga kuweka
hivyo viwanda hapa kwa sababu tuna eneo la kutosha.”
Hata
hivyo, Bw. Kiluwa alitumia fursa hiyo kumweleza Waziri Mkuu kwamba
wanapata taabu ya makaa ya mawe kwa sababu wanaletewa makaa yenye ukubwa
wa milimita 10 hadi 15 badala ya milimita 35 – 40 ambazo wanahitaji kwa
ajili ya kiwanda chao.
“Tukiagiza
tani 30, tunachambua mawe ya saizi inayotufaa na kujikuta tunabakia na
tani saba tu. Kiasi kilichobakia ni vumbi tupu,” alisema.
Waziri
Mkuu alimwagiza Naibu Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara, Eng. John
Malongo awasiliane na Wizara ya Nishati na Madini ili afuatilie ni kwa
nini watengenezaji wa makaa ya mawe hawafuati vipimo halisi
vinavyotolewa na wawekezaji.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
No comments:
Post a Comment