
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameliagiza jeshi la Magereza na idara zingine zenye mashirika ya uzalishaji ambazo zipo chini ya wizara yake zifanye uzalishaji mali pamoja na kuwatumia wafungwa katika kufanya kazi ndani ya jeshi.
Waziri
Nchemba ameongea hayo akiwa katika ufunguzi wa nyumba tano za maaskari
wa jeshi la magereza mkoa wa Arusha nyumba zilizojengwa kwa kutumia
fedha za shirika la magereza la uzalishaji mkoani humo.
Mh.
Nchemba ametoa rai kwa jeshi hilo kuona kama inawezekana jeshi hilo
kutumia wafungwa ambao wamemaliza mafunzo yao na wakaona wamerekebika
kitabia na kuwachukua waendelee kufanya kazi kwa mkataba katika
mashirika hayo kwani itarahisisha kupunguza wahalifu zaidi kuliko kwenda
uraiani wakiwa hawana uwezo wakufungua biashara na kurudia makosa.
Naye
mkuu wa Magereza Tanzania Dr Juma Malewa amewataka wananchi na
mashirika ya umma na serikali kutumia jeshi la Magereza nchini katika
shughuli za ujenzi kwani gharama zake ni nafuu sana lakini zenye ubora
zaidi.
Kwa
upande wa Mkuu wa Jeshi la Magereza mkoa wa Arusha, Hamis Nkabasi
amesema nyumba hizo zimetumia gharama ndogo za ujenzi kwasababu
rasilimali watu wametumia askari wenye ujuzi wa ujenzi na wafungwa
ambapo imegharimu milioni 50 kila nyumba na itaweza kuchukua askari 12
ambapo zote zitachukua askari 60 na kama wangechukua kampuni kujenga
basi ingegharimu fedha nyingi zaidi.
No comments:
Post a Comment