Jupp Heynckes aweka rekodi ambayo hakuna Mjerumani anayemsogelea - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, November 20, 2017

Jupp Heynckes aweka rekodi ambayo hakuna Mjerumani anayemsogelea



Mwaka 2013 kocha wa sasa wa Bayern Munich Jupp Heynckes aliweka rekodi nchini Ujerumani baada ya kuwa kocha wa kwanza nchini Ujerumani kubeba Bundesliga,Dfb Cup na Champions League katika msimu mmoja.

Lakini wikiendi hii kocha huyo kwa mara nyingine ameweka rekodi nyingine kubwa ndani ya ardhi ya Ujerumani baada ya kuwa kocha wa mtu wa  kwanza kushinda mechi 500 za ligi hiyo kama mchezaji na kocha.

Ushindi zidi ya ulikuwa mchezo wa Heynckens wa 1016 kama mchezaji/kocha na huo ukawa ushindi wake wa 326 akiwa kama kocha Bundesliga huku hapo kabla akishinda michezo 174 kama mchezaji.

Tarehe 14 August mwaka 1965 ndipo ambapo safari ya Heynckens katika rekodi hii ilianza na huo ukiwa msimu wa 3 tu wa Bundesliga akiwa anaichezea Glabach ambapo wiki tu baada ya kuanza soka alifunga bao lake la kwanza.

Mwaka 1974 Heynckens alikuwepo wakati Glabach wakiifunga Dortmund mabao 12 kwa 0 rekodi ya ushindi mkubwa kati Bundesliga na Heynckens alifunga mabao 5 katika mchezo huo lakini mwaka huo huo ndio mwaka alioacha kucheza soka.

Toka Jupp Heynckens arudi tena kuifundisha Bayern Munich akichukua mikoba Carlo Anceloti klabu hiyo imekuwa na matokeo mazuri sana na sasa wako kileleni wakiongoza ligi kwa alama 32.

No comments:

Post a Comment