Tuunaamini katika rekodi/historia? Kama ni hivyo baasi Barcelona ni bingwa wa La Liga msimu huu - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, November 20, 2017

Tuunaamini katika rekodi/historia? Kama ni hivyo baasi Barcelona ni bingwa wa La Liga msimu huu

Wikiendi hii michuano ya La Liga iliendelea ambapo miamba mitatu Atletico Madrid, Real Madrid na Barcelona walikuwa uwanjani. Madrid Derby iliisha kwa suluhu na kuipa Barcelona uongozi mpana wa ligi.

Suluhu kati ya Atletico Madrid na Real Madrid imewafanya wote wawili kubaki na alama 24, Barcelona ambao ni vinara wa ligi wana alama 34 ikiwa ni tofauti ya alama 10(michezo minne) na wababe hao wawili.

Tangu michuano ya La Liga ianze ni mara saba tu ambapo kinara wa ligi aliiacha timu nyingine kwa
idadi hiyo ya alama ikiwa sawa na michezo minne na kisha pengo hilo la alama likazibwa na timu iliyoliziba ikachukua ubingwa.

Na Barcelona ambao ndio vinara wa michuano hii hadi sasa ndio wanaonekana kuwa na uwezo wa kuziba tofauti ya alama za mechi 4 kwani kati ya mara hizo 7 wameshafanya mara nne huku Real Madrid wakiwa hawajawahi kuziba pengo la alama kama hizo.

Msimu wa La Liga 1928/1929 Real Madrid walikuwa wakiongoza kwa tofauti ya alama 12 zikiwa zimebaki mechi 11 ambapo ina maana kulikuwa kuna alama 22 za kuchukua( alama zilikuwa 2 ukishinda mechi) na Barcelona walifanikiwa kuziba pengo hilo na kubeba kombe.

Msimu wa mwaka 1949/1950 Real Madrid wakafanya tena kilekile cha 1928/1929. Safari hii ilikuwa na Atletico Madrid,hadi inafika mechi ya 13 Real Madrid walikuwa wana alama 19 huku Atletico wakiwa na 12 lakini ligi ikaisha Atletico wakiwa na alama 33 huku Real wakiishia 31.

1951/1952 ikawa zamu ya Atletico Madrid , Atletico waliongoza ligi zikiwa zimebaki mechi 23 (alama 46) lakini katika michezo hiyo iliyobaki Barcelona waliokuwa nafasi ya 5 wakiachwa alama 7 na vinara wa ligi walichukua alama 37 na Atletico wakichukua 24, Barcelona akawa bingwa.

Barcelona tena 1952/1953 wanawafanyia Espanyol kile walichowafanya Atletico Madrid msimu uliopita, mchezo wa 16 Espanyol walikuwa wakiongoza ligi wakiwa na alama zao 26 huku Barcelona wakiwa nafasi ya 5.

Barcelona walikuwa nafasi hiyo ya 5 wakiwa na tofauti na alama 7 na vinara Espanyol lakini Barcelona wakabeba alama 23 kati ya 28 zilizokuwa zimebaki huku Espanyol wakikusanya alama 10 tu na Barcelona akatangazwa bingwa.

Mwaka 1981 Real Sociedad nao walikuwa nyuma kwa alama 7 toka walipo vinara wa ligi mwaka huo Atletico Madrid ikiwa ni mechi ya 18 lakini Real Sociedad waliziba tofauti ya alama hizo na kubeba ubingwa La Liga.

Barcelona tena 1991/1992 ambapo mchezo wa 14 tu wa ligi walikuwa tayari wana tofauti ya alama nane na Real Madrid lakini ikashuhudiwa La Liga ikiisha huku Barcelona wakitawazwa mabingwa wa michuano hiyo.

Sasa ni miaka 24 imepita tangu mara ya mwisho timu itoke nyuma ya alama ambazo ni sawa na michezo minne na kuziba alama hizo na kisha kuchukua ubingwa(kumbuka zamani ushindi ilikuwa alama 2), bado michezo 26 ya La Liga na labda Real Madrid wataweza kufanya kile ambacho hawakukiweza awali.

No comments:

Post a Comment