![]()

Lionel Messi amefunga jumla ya magoli 16 katika mechi 18 alizocheza
msimu huu, lakini anasafiri Jumanne hii kuelekea jijini Turin Italia
akiwa na ukame wa mwaka mzima; hajafunga goli katika michuano ya
Champions League kwenye mechi zilizochezwa ugenini kwa kipindi cha
takribani mwaka sasa.
Messi anahitaji magoli mawili kuweza kutimiza magoli 100 katika
mashindano ya ulaya lakini mara ya mwisho kwake kufunga eneo tofauti na
Nou Camp katika UCL ilikuwa wakati alipofunga magoli mawili dhidi ya
Celtic jijini Glasgow mnamo November 23 mwaka jana.

Tangu
hapo, Messi amecheza mechi 4 za ugenini lakini ameshindwa kufunga
katika mechi hizo zote. Msimu uliopita, alishindwa kufunga katika mechi
za vipigo vya 4-0 vs PSG na 3-0 vs Juventus. Msimu tayari Barca
wameshasafiri mara 2, wamecheza dhidi ya Sporting club de Portugal na
Olympiakos na mechi zote hizo ukame wa Messi uliendelea.

Katika mechi 4 zilizopita za mashindano yote – La Purga hajaona nyavu
hata mara moja. Mara ya mwisho kufunga goli ilikuwa katika dimba la San
Mames mnamo Oktoba 28 mwaka huu, lakini ameshindwa kuwafunga Leganes,
Sevilla, Olympiakos na Russia ambayo alicheza nayo akiwa na Argentina.
No comments:
Post a Comment