Mshindi wa michuano ya Wimbledon afariki dunia - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, November 20, 2017

Mshindi wa michuano ya Wimbledon afariki dunia


Aliyekuwa mshindi wa michuano ya Wimbledon mwaka 1998 raia wa Uswisi Jan Novotna amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na matatizo ya kansa.

Novtna amefariki nchini kwao Czech Republic akiwa amezungukwa na familia yake, Novtana atakumbukwa kwa ubora wake miaka ya 90 akishinda makombe binafsi 24 tangu aanze tennis.

Mwaka 1997 Novtna alipoteza katika michuano ya Wimbledon kwa kutolewa na Marina Hingis lakini mwaka mmoja baadae ilipofika 1998 alilipa kisasi kwa kumtoa Hingis katika nusu fainali kisha kumshinda Nathalie Tauzat katika fainali.

Katika enzi z uhai wake Novotna amewahi kuingia katika fainali moja ya Australian Open na French Open, huku akiingia fainali za Us Open mara mbili na akifanikiwa kushinda grand slam 12.

No comments:

Post a Comment