
Bado kesi ya kutumia vibaya ofisi za FIFA inaunguruma na hii leo mashahidi kadhaa walipanda kizimbani kutoa ushahidi wao juu ya masuala ya rushwa yanayotajwa kuligubika shirika hilo wakati wa utawala wa Sepp Blatter.
Kubwa lililojiri ni taarifa mpya kuhusu makamau wa zamani wa Sepp Blatter bwana Julio Grondona ambaye imetajwa mahakamani hapo kwamba alipewa kiasi cha $1m kwa ajili ya kuipigia kura Quatar.
Akiongea mahakamani hapo Julio Curzao ambaye ni mkurugenzi wa kampuni moja inayohusika na masuala ya masoko katika michezo alisema Grondona alimuambia kuhusu kiasi hicho.
Curzao anasema mwanzoni hakufahamu kiasi hicho cha pesa kinatokea katika nchi gani lakini baada ya Grondona kubadili mawazo na kusema anaipigia kura Quatar ndipo akafahamu pesa hiyo inakotoka.
Grondona anatajwa kuwa alikuwa akicontrol mchakato huo wa rushwa huku yeye na mjumbe mwingine aitwaye Teixeira ambaye naye aliipigia kura Quatar huku mjumbe mwingine toka Paraguay akikataa suala hilo na kuamua kuipigia kura Japan.
Grondona pia alijaribu kwenda hadi kwa maofisa wa FIFA katika nchini nyingine ikiwemo nfani ya Urusi kujaribu kuwashawishi kupiga kura kwa ajili ya Quatar kuandaa michuano hiyo mikubwa mwaka 2022.
Quatar wameshakana kwa mara kadhaa tuhuma hizi zinazoelekezwa juu yao huku wakisisitiza kwamba mchakato ulikuwa wa haki, Quatar ndio waandaaji wa michuano ya kombe la dunia 2022.
No comments:
Post a Comment