Lakini Halep alifanya kile ambacho mashabiki wengi walitamani afanye kwa kumpiga Angelique ambaye alikuwa bingwa mwaka 2016 kwa kumchapa kwa seti 6-3 4-6 na 9-7.
Sasa Halep atakutana na Caroline Wozniacki ambaye alimtoa Elise Martens katika nusu fainali ya kwanza, na fainali itapigwa siku ya Jumapili kumpata bingwa wa Australia Open kwa upande wa kina dada.
Halep ambaye anashirikia nafasi ya kwanza katika viwango vya tennis kwa upende wa wanawake alikiri baada ya mchezo huo kwamba mchezo ulikuwa mgumu zaidi kwake katika michuano hiyo.
Halep pamoja na Kerber waliingia katika fainali hii huku wote wawili wakiwa wamecheza michezo 10 katika mwaka huu 2018 na hakuna hata mmoja aliyewahi kupoteza.
No comments:
Post a Comment