Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 30, 2021 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jeshi, Upanga jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Habari Jeshini, Gaudentius Ironda, amesema matapeli hao wameenda mbali zaidi na kutumia jina la mkuu wa majeshi, wakieleza kwamba ndiye aliyewatuma kukusanya fedha ili wapate nafasi ya kuandikishwa, jambo ambalo si la kweli.
Amewataka wananchi kutoa taarifa haraka endapo watakutana na watu wa aina hiyo, na kusisitiza kwamba jeshi halina utaratibu wa kuwatoza watu fedha ili wapate nafasi ya kujiandikisha na kwamba wanaofanya vitendo hivyo ni matapeli.
No comments:
Post a Comment