| Meja Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko Mwenyekti wa bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa wanyama Pori Tanzania [TAWA] |
Na.Okuly Julius,Dodoma.
Waziri wa Utalii Dkt.Damas Ndumbaro amewataka wawekezaji wazawa pamoja na wa kigeni kuchangamkia fursa za uwekezaji wa uwindaji na utalii ili kuimarisha maliasili na kukuza uchumi wanchi.
Dkt.Ndumbaro amebainisha hayo jijini Dodoma wakati wa utoaji wa tuzo za umahiri pamoja na cheti kwa kampuni nne za Green Nile Safari LTD,Grumet Services Ltd,Mwiba Holding LTD,na kampuni ya ndani ya Mkwawa Hunting Safari katika uwekezaji wa uwindaji na utalii kwa wanyamapori zilizoandaliwa na mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania [TAWA].
Dkt.Ndumbaro amesema serikali itaendelea kutoa fursa kwa wawekezaji kwenye sekta ya utalii pamoja na kuendelea kuboresha huduma za kitalii nchini ikiwemo upatikanaji wa leseni ya shughuli za utalii kwa uharaka Zaidi pamoja na mifumo ya malazi.
Aidha.Dkt.Ndumbaro ametumia fursa hiyo kuipongeza mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori [TAWA]kwa kuendelea kusimamizi uhifadhi wa wanyamapori nchini.
Kuhusu suala la uvamizi wa maeneo ya uhifadhi kutokana na shughuli za binadamu Dkt.Ndumbaro ameitaka TAWA kuendelea kujiimarisha Zaidi hali itakayosaidia kuendelea kulinda na kuhifadhi maeneo muhimu ya uhifadhi.
Mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa wanyama Pori Tanzania [TAWA] Meja Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko amesema Matarajio ni ukusanyaji wa Zaidi ya Tsh.Bilioni 23 kwa mwaka kutokana na uwekezaji wa kampuni 4 kwenye nyanja ya uwindaji na utalii
Aidha,amesema Bodi hiyo itaendelea kusimamia vyema katika kuhakikisha mapato yatokanayo na wanyamapori yanawanufaisha watanzania
Wakizungumza mara baada ya kutunukiwa vyeti hivyo mwakilishi kampuni ya GREEN NILE SAFARI’S LTD SELEM BAILEITH amesema atajitahidi katika kuimarisha uwindaji na uhifadhi wa wanyamapori huku mwakilishi wa kampuni ya Mkwawa Hunting SAFARI ,BENSON akisema wazawa wanaweza katika masuala mazima ya uwekezaji wa uwindaji na uhifadhi wa wanyamapori katika sekta ya utalii.
Pia ,amesema moja ya changamoto wanayokumbana nayo ni katika hifadhi ya Selous ambapo nyakati za masika njia huwa hazipitiki ila wameahidi kama Mkwawa Hunting Safaris watatatua changamoto hiyo.
Ikumbukwe kuwa utaratibu wa kuwapata wawekezaji kwa njia ya SWICA [Special Wildlife Invenstment Concession Areas ] ulifanyika kwa mujibu wa kanuni za SWICA mwaka 2020 ambazo zimempa mamlaka kamishna wa uhifadhi,TAWA ,kuunda timu ya majadiliano na hii ilikuja baada ya wizara ya Maliasili kufanya utafiti katika nchi za Botswana,Afrika Kusini, Msumbiji na Madagascar kwani kufuatia utafiti huo ulibaini kuwa mpango huu una tija katika kuongeza mapato yatokanayo na shughuli za utalii na unaruhusu uwekezaji wa miaka 30 hivyo utatoa fursa kwa wawekezaji kufanya shughuli za utalii wa picha na uwindaji wa kitalii ndani ya maeneo yaliyotengwa.



No comments:
Post a Comment