Na Mwandishi wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Innocent Bashungwa amemuelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Prof.Riziki Shemdoe kuwashusha vyeo Wakuu wa Vitengo vya Manunuzi na Ugavi 23 kutoka kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini.
Mhe. Bashungwa ametoa maelekezo hayo baaada ya kufanyika kwa tathmini ya utendaji kazi kwa baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa kama iliyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa ziara yake mkoani Mara Februari 05, 2022.
Tathmini iliyofanywa ililenga kupima uhalisia wa utendaji kazi wa Wakuu wa Idara na vitengo katika utoaji wa huduma na utekelezaji wa shughuli za maendeleo,ujazaji wa nafasi wazi za Wakuu wa Idarana Vitengo,kuboresha na kuondoa changamoto za utoaji wa huduma katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Tathmini ya utendaji kazi wa Wakuu wa Vitengo vya Manunuzi na Ugavi imefanyika ili kubaini utendaji kazi wa watumishi hao katika kusimamia masuala mbalimbali ya ununuzi wa Umma.
Baada ya tathimini hii kukamilika katika Kitengo cha Manunuzi na Ugavi hatua mbalimbali zimechukuliwa zenye lengo la kuimarisha utendaji kazi ambapo Prof. Shemdoe amewashusha vyeo na kuwapangia majukumu mengine Wakuu wa Vitengo vya Manunuzi 23 ambao wamethibitika kuwa utendaji kazi wao haukuwa wa kuridhisha.
Prof. Shemdoe amebainisha kuwa wapo watumishi ambao hatua za kinidhamu na jinai zinaendelea kuchukuliwa dhidi yao na watachukuliwa hatua stahiki kulingana na matokeo ya kesi
zao.
Aidha amesema kuwa ili kuendelea kuimarisha utendaji kazi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa tathmini kama hizi zitaendelea kufanyika kwa watumishi wa kada zingine.
Pia amewaelekeza Makatibu Tawala Mikoa na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuendelea kuchukia hatua za kinidhamu kwa watumishi wote wanaokiuka maadili ya Utumishi wa Umma kwenye maeneo yao.
Orodha ya majina ya Wakuu wa Vitengo vya Manunuzi na Ugavi waliovuliwa madaraka imeambatanishwa.
1.ARUSHA CC,Kilanga Edward Mangwala,Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi
2.Monduli DC,Jeremia Makweba Ryatula,Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi
3.Dodoma CC,Ellyhuruma Mutta Mufuruki,Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi
4.Geita TC,Patric Ndaba,Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi
5.Geita DC,Joash F. Kunaga,Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi
6.Kyerwa DC,Alex Iginatus Kaganda,Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi
7.Kigoma DC,Maria Paul Silayo,Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi
8.Same DC,Hamadi Hamisi Mfinanga,Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi
9.Siha DC,Suleiman Ramadhan Mpanju,Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi
10.Butiama DC,Chaina Mwita Masamaki,Afisa Ugavi Mwandamizi
11.Busokelo DC,Malick John Panjo,Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi
12.Kyela DC,Janet Nswila Patrick,Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi
13.Mbarali DC,Michael Mugisha Kasenene,Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi
14.Mvomero DC,Peter Lebarwa,Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi
15.Mwanza CC,Biseko Mkama Makori,Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi
16.Buchosa DC ,Agai Benjamin Kisare ,Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi
17.Chalinze DC ,Anne Daudi Mwandiga ,Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi
18.Kisarawe DC ,Alexander Martin Chang’a ,Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi
19.Mkuranga DC ,Beda Faustine Mmbaga ,Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi
20.Itigi DC Patric Y. Kagere
21.Korogwe DC ,Geofrey A. Matandiko ,Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi
22 .Handeni TC ,Wilbard V. Sakaya Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi
23 .Pangani DC, Mfaume A. Mchengwa ,Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi


No comments:
Post a Comment