Hospitali ya Benjamin Mkapa kujenga jengo maalumu kwa ajili ya Kliniki ya Saratani. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, March 14, 2022

Hospitali ya Benjamin Mkapa kujenga jengo maalumu kwa ajili ya Kliniki ya Saratani.




Na Mwandishi wetu, Dodoma 
Hospitali ya Benjamin Mkapa kujenga jengo maalumu kwa ajili ya Kliniki ya Saratani kwa lengo la kusaidia watanzania kutosafiri umbali mrefu kutafuta huduma hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji Dkt.Alphonce Chandika ameyasema hayo mwishoni mwa wiki ilitopita jijini Dar es Salaam katika kipindi maalumu cha mwaka mmoja wa Rais samia kinacho endeshwa na TBC1.

"Napenda kutoa shukrani za dhati kabisa kwa namna Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anavyo endelea kutushika mkono katika ukuaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kwani alipo ingia madarakani ametupatia kibali cha kuanza kujenga jengo la matibabu ya saratani na kwakuanza ametutengea bajeti ya bilioni mbili"

Dkt. Chandika amesema kwa sasa wagonjwa wa saratani wanalazimika kwenda umbali mrefu kupata matibabu ya saratani. 

"Jengo hilo mpaka litakapo kamilika litagharimu jumla bilioni 27, jengo hililikikamilika litawasaidia wagonjwa wa Saratani kanda ya kati" alisema Dkt Dkt Alphonce



No comments:

Post a Comment