KIKAO KAZI CHA KUPITIA RASIMU YA MPANGO WA TAIFA WA UTEKELEZAJI WA AHADI ZA NCHI KATIKA JUKWAA LA KIZAZI CHENYE USAWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, April 29, 2022

KIKAO KAZI CHA KUPITIA RASIMU YA MPANGO WA TAIFA WA UTEKELEZAJI WA AHADI ZA NCHI KATIKA JUKWAA LA KIZAZI CHENYE USAWA


Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Zainab Chaula akiongoza Menejimenti ya Wizara kupitia Mpango wa Taifa wa utekelezaji wa ahadi za nchi katika Jukwaa la kizazi chenye Usawa.(GEF),Ofisini kwake jijini Dodoma leo tarehe 29/04/2022. Kikao hicho kimehudhuriwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri na Uratibu katika Utekelezaji wa ahadi za nchi kwenye Jukwaa la kizazi cha Usawa Angellah Kairuki.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia, Mwajuma Magwiza akiwasilisha taarifa ya hatua zilizofikiwa katika uratibu wa utekelezaji wa ahadi za nchi kwenye Jukwaa la kizazi cha usawa katika kikao cha kujadili hatua hizo, kilichohudhuriwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Utekelezaji na Uratibu wa ahadi za nchi katika Jukwaa la kizazi cha usawa Angellah
Kairuki.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Amon Mpanju akizungumza na Menejimenti ya Wizara kupitia Mpango wa Taifa wa Utekelezaji wa ahadi za nchi katika Jukwaa la kizazi cha usawa. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Jinsia, Badru Abdulnuru akiwasilisha rasimu ya Mpango wa utekekezaji wa ahadi za nchi katika Jukwaa la Kizazi chenye usawa, wakayi wa Kikao cha Menenjimenti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, kikao hicho kimehudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri na Uratibu wa Utekelezaji wa ahadi za nchi katika Jukwaa la kizazi chenye usawa Angellah Kairuki.
Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum wakifuatilia wasilisho la hatua zilizofikiwa katika uratibu wa utekelezaji wa ahadi za nchi katika Jukwaa la Kizazi chenye usawa(GEF), kutoka kwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia Mwajuma Magwiza.

No comments:

Post a Comment