 |
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, akizundua mashine ya kielektroniki ya ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali yatokanayo na makosa ya usalama barabarani katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma, leo Aprili 27, 2022. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio, na wapili kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. |
 |
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, akionyesha mashine ya kielektroniki ya ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali yatokanayo na makosa ya usalama barabarani baada ya kuizindua katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma, leo Aprili 27, 2022. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio, na wapili kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. |
 |
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, akizungumza na viongozi wa Jeshi la Polisi, Maafisa mbalimbali wa Wizara yake baada ya uzinduzi wa mashine ya kielektroniki ya ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali yatokanayo na makosa ya usalama barabarani katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma, leo Aprili 27, 2022. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. |
 |
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, akizungumza na viongozi wa Jeshi la Polisi, Maafisa mbalimbali wa Wizara yake (hawapo pichani) baada ya uzinduzi wa mashine ya kielektroniki ya ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali yatokanayo na makosa ya usalama barabarani katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma, leo Aprili 27, 2022. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. |
 |
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini (katikati), akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio, alipokuwa akizungumza katika haflaya uzinduzi wa mashine ya kielektroniki ya ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali yatokanayo na makosa ya usalama barabarani iliyofanyika jijini Dodoma, leo Aprili 27, 2022. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. |
 |
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mashine ya kielektroniki ya ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali yatokanayo na makosa ya usalama barabarani iliyofanyika jijini Dodoma, leo Aprili 27, 2022. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, na wapili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. |
 |
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini (katikati meza kuu), akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara hiyo baada ya uzinduzi wa mashine ya kielektroniki ya ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali yatokanayo na makosa ya usalama barabarani, jijini Dodoma, leo Aprili 27, 2022. Kushoto meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio, na kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. |
Na Okuly Julius Dodoma
NAIBU WAZIRI wa Wizara ya Mambo ya ndani Mhe.Jumanne Sagini amewataka Wamiliki na Watumiaji wa vyombo vya moto barabarani kuzingatia na kufuata sheria za usalama barabarani ikiwemo kulipa madeni wanayodaiwa bila kushurutishwa.
Ameyasema hayo leo April 27,2022 Jijini Dodoma wakati akizindua Mashine mpya za kisasa za (POS) kwa ajili ya kukusunyia Maduhuli ya jeshi la polisi hususani kitengo cha usalama barabarani pamoja na kutumika katika ununuzi wa silaha,Hati ya tabia njema na kukusanyia tozo mbalimbali barabarani hasa kwa madereva wasiofuata sheria za usalama barabarani.
Mhe.Sagini Ameongeza kuwa Mashine hizo mpya zina tumia mfumo wa Android hivyo ina Wireless, inaskani leseni,inauwezo wa kuchukuwa alama za Vidole pamoja na kupiga picha jambo ambalo litasaidia kupunguza malalamiko ya wananchi yaliyokuwepo.
Hivyo amewapongeza Jeshi la polisi nchini kwa kutumia wataalamu wake wa ndani kuendeleza mfumo huo ambao unakwenda kupunguzia jeshi hilo malalamiko na kuwafanya waweze kutekeleza majukumu yao bila kutumia nguvu kubwa kwa sababu mfumo huu kwa sasa unachukuwa taarifa za muhimu kwa Dereva hivyo hawezi kuja kukataa kwa sababu alama za vidole havifanani dunia nzima.
"Nawapongeza sana naamini mfumo huu utakwenda kuwa chanya kwenu na kwa wananchi hatutegemei kupata malalamiko tena ya kuwepo kwa makosa katika kumuandikia mtu kosa "Amesema Mhe,Sagini
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro amewataka watumiaji wa barabara hususani madareva kutii sheria bila shuruti na kutoa ushirikiano pale Askari wa usalama barabarani wanapotaka kuchukua taarifa zao kwa ajili ya kujiridhisha wanapoandika ama kufanya ukaguzi wa vyombo vya moto.
"Kwa mashine hizi mpya inahitaji dereva achukuliwe alama za vidole,picha na kuskani leseni sasa niwaombe usiwe mbishi pale askari anapotaka taarifa hizi mtoe ushirikiano kikubwa tii sheria bila kushurutishwa"Amesema IGP Sirro
Naye Mkuu wa kitengo cha TEHAMA (ICT) wa jeshi la polisi nchini ACP.Dawson Msongaleli amesema kuwa mfumo huo ulianza kwa kufanyiwa majaribia kwa mkoa wa Dar-es-salaam na Pwani mwaka 2017 baada ya kufanya kazi vizuri ndipo 2018 wakaanza kutumia kwa mikoa yote ya Tanzania Bara.
Amemaliza kuwa nia ya kutumia mashine hizi ni kuondokana na ule mfumo wa kujazana katika vituo vya polisi na kusababisha foleni isiyokuwa na maana na badala yake kila kitu kitafanyika kielektroniki.
No comments:
Post a Comment