TAKUKURU MKOA WA DODOMA WAENDELEA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA KUTOA ELIMU KWA WAKAZI WA DODOMA, WAWAKUMBUSHWA WAJIBU WA KUSHIRIKI KUZUIA VITENDO VYA RUSHWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, April 29, 2022

TAKUKURU MKOA WA DODOMA WAENDELEA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA KUTOA ELIMU KWA WAKAZI WA DODOMA, WAWAKUMBUSHWA WAJIBU WA KUSHIRIKI KUZUIA VITENDO VYA RUSHWA


Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Sosthenes W.Kibwengo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma mapema leo Aprili 29,2022 katika ofisi za TAKUKURU mkoa wa Dodoma
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Sosthenes W.Kibwengo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma mapema leo Aprili 29,2022 katika ofisi za TAKUKURU mkoa wa Dodoma
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Sosthenes W.Kibwengo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma mapema leo Aprili 29,2022 katika ofisi za TAKUKURU mkoa wa Dodoma

Na Okuly Julius Dodoma 

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma, imeendelea na utekelezaji wa majukumu yake katika robo ya Januari hadi Machi, 2022 ambapo mkazo uliwekwa katika KUZUIA RUSHWA.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Sosthenes W.Kibwengo amesema Kazi zilizofanyika ni pamoja na kutoa elimu ya kuhamasisha wananchi ili washiriki kikamilifu katika kuzuia rushwa kwakuwa rushwa huzorotesha maendeleo ya jamii jambo ambalo limefanyika kikamilifu.

Pia Sosthenes Kibwengo amesema katika kulinganisha kazi za Uelimishaji kwa Umma zilizofanyika katika robo kama hii mwaka jana, kuna ongezeko la asilimia 115 la kazi zilizofanyika kwa robo ya mwaka huu.

Ameongoza kuwa elimu dhidi ya rushwa ilitolewa kupitia Semina 50, Maonesho 5,Vipindi vya redio 18 na kipindi kimoja cha televisheni hivyo anaamini kuwa Uelimishaji huo umesaidia kuwafungua fikra watanzania kuhusu mapambano dhidi ya rushwa.

Ppamoja na hayo amegusia katika eneo la UZUIAJI RUSHWA na kwa kuzingatia kwamba Miradi ya Maendeleo ni mali ya wananchi na Serikali inapeleka fedha nyingi katika eneo hilo,TAKUKURU Mkoa wa Dodoma imefuatilia utekelezaji wa miradi arobaini na moja (41) yenye thamani ya shilingi bilioni 11.2, katika sekta za Ujenzi, Elimu, Afya na Maji. Hii inajumuisha miradi ya Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya UVIKO 19.

"Miradi 10 (sawa na asilimia 24), ilikutwa na mapungufu madogo kama ya kuchelewa kukamilishwa kwa mujibu wa mkataba, jambo linalosababisha kuongezeka kwa gharama, matumizi ya vifaa visivyokidhi ubora,pamoja na manunuzi kwa gharama zaidi ya bei ya soko,"Amesema Sosthenes W.Kibwengo na kuongeza kuwa

"Mapungufu husika yalirekebishwa kwa kutoa elimu na kusimamia marekebisho kwa kushirikiana na wadau," Amesema

Amesema Mradi mmoja ulionekana kuwa na viashiria vya jinai na hivyo uchunguzi umeanzishwa na shilingi milioni 409.4 zilizolipwa kwa Mkandarasi kinyume na taratibu katika utekelezaji wa mradi mmoja zilirejeshwa kwa kushirikiana na halmashauri husika na hiyo ni moja kati ya hatua zinazoendelea kuchukuliwa na TAKUKURU mkoa wa Dodoma.

"Tumebaini kwamba, pamoja na mambo mengine, kuna utitiri wa leseni za uchimbaji wa madini na ujenzi, lakini maeneo mengi hakuna kinachoendelea na hivyo kuzinyima halmashauri mapato. Mfano wilayani Mpwapwa kuna leseni za wachimbaji 773 lakini zinazotumika ni 57 tu,"Ameongeza Sosthenes W.Kibwengo

Pia halmashauri zinapoteza mapato katika maeneo ambayo uchimbaji unafanyika kiholela na ambayo hayana Mashine za Kielektroniki za kukusanya ushuru - Point of Sale - POS.

Kwenye uchambuzi wa mfumo wa viashiria vya rushwa ya ngono katika sekta ya Elimu ngazi ya halmashauri, imebainika kuwa maeneo hatarishi kwa uwepo wa rushwa ya ngono ni katika Upangaji wa vituo vya kazi kwa asilimia 72 na Uhamisho ndani ya halmashauri kwa asilimia 63.

Kwenye uchambuzi wa mfumo wa ujenzi wa Shule Shikizi, imebainika kuwa kuna ufahamu mdogo kwa Kamati za Shule kuhusu matumizi ya mfumo wa manunuzi wa 'force account'.

pia tutaendelea kufuatilia makusanyo na uwasilishaji wa mapato yanayotokana na vyanzo mbalimbali ili kuzuia ubadhirifu na kuchukua hatua stahiki kwa wale watakaobainika kufuja mali za umma.

Amemalizia kwa kuwasihi wengine wote wenye mtazamo kwamba kazi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ni ya Serikali pekee waachane na fikra hizo batili na wajiunge kuongeza nguvu katika umoja wa wazalendo, waadilifu na wanaojisikia fahari kuzuia rushwa. Umoja ni nguvu. RUSHWA HAILIPI


No comments:

Post a Comment