WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA MAANDALIZI KUELEKEA SHEREHE ZA MEI MOSI -OKULYBLOG - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, April 30, 2022

WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA MAANDALIZI KUELEKEA SHEREHE ZA MEI MOSI -OKULYBLOG


Waziri mkuu Kassim Majaliwa

Na Okuly Julius Dodoma

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa ameridhishwa na maandalizi kuelekea siku ya Mei Mosi yatakayofanyika kitaifa jijini Dodoma ambapo ameitaka kamati ya maandalizi kuhakikisha wanakamilisha mambo machache yaliyosalia mpaka kufikia jioni ya Aprili 30,2022.

Ameyasema hayo wakati alipotembelea uwanja wa Jamhuri Dodoma kukagua maandalizi na kupokea ripoti ya kamati hiyo huku akiipongeza na kusema kuwa imefanya kazi nzuri hivyo wajitahidi kuangalia seheme zenye changamoto na kuzitatua mapema ili kufanya maandalizi kuwa asilimia mia moja.

"Nakiri kwamba nimefika na nimeridhika ,nimejionea maandalizi mazuri niwapongeze kamati ikiongozwa na Waziri wa nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia kazi,ajira,vijana na wenye ulemavu Prof Joyce Ndalichako kazi yenu inakwenda vizuri niombe tu muendelee kushirikiana vizuri na kamati kuhakikisha mnakamilisha maandalizi yote",Amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Pia amewataka kuzingatia muda katika upangaji wa ratiba yao na kufupisha baadhi ya matukio wakizingatia huu ni Mwezi wa sikukuu hivyo hakuna haja ya kukaa muda mrefu ili kutoa mwanya kwa Wananchi waliofunga kujiandaa na Sikukuu ya Ramadhani.

"Tujitahidi kufuata ratiba na kufupisha baadhi ya mambo tutambue kuwa huu ni mwezi wa sikukuu hivyo kuna haja ya kufanya tukio hili mapema ili tuwape muda ndugu zetu Waislamu wa kuendeleà na maandalizi yao ya Sikukuu,"Amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia kazi, ajira, vijana na wenye ulemavu Prof Joyce Ndalichako amesema kuwa maandalizi yamekamilika zaidi ya asilimia 90% hivyo maandalizi madogo mpaka kufikia jioni yatakuwa yamekamilika hivyo imani ni kuwa Mei Mosi ya kesho itakuwa ni bora zaidi.

No comments:

Post a Comment