- OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, April 30, 2022



Waziri wa Habari Mawasiliano, Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) akizungumza wakati wa mkutano wake na wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika leo Aprili 30, 2022 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akizungumza wakati wa mkutano wa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Nape Nnauye (hayupo pichani) na wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika leo Aprili 30, 2022 jijini Dodoma.
Dkt. Revocatus Baltazar kutoka ofisi ya Mganga Mkuu wa jiji la Dodoma akitoa mada kuhusu magonjwa yasiyoambukiza wakati wa mkutano wa Waziri wa Wizara wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (hayupo pichani) na wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika leo Aprili 30, 2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Habari Mawasiliano, Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi wakati wa mkutano wake na wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika leo Aprili 30, 2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bi. Teddy Njau akizungumza wakati wa mkutano wa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Nape Nnauye (hayupo pichani) na wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika leo Aprili 30, 2022 jijini Dodoma.
Mwenyekiti TUGHE wa Tawi la Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Laurencia Masigo akizungumza wakati wa mkutano wa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Nape Nnauye (hayupo pichani) na wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika leo Aprili 30, 2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi la Wizara hiyo baada ya mkutano wake na wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika leo Aprili 30, 2022 jijini Dodoma.

Na Okuly Julius Dodoma 

WAZIRI wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amewataka wafanyakazi Wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa bidii na weledi kwa kuzingatia misingi ya sheria haki na ustawi kwa wateja wanaowahudumia.

Waziri Nape ameyasema hayo leo Aprili 30 jijini hapa katika kikao cha wafanyakazi na Serikali na afya TUGHE ambapo amesema baadhi ya watumishi wa umma wanafanya kazi kwa mazoea hali inayoathiri uwajibikaji wa pamoja katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

“Ninawaomba Watumishi tuache kufanya kazi kwa mazoea, ondokeni katika kufanya kazi kwa analojia na badala yake tuhakikishe tunafanya kazi zitakazoacha alama,

“ Kila binadamu ana vipawa ambavyo Mungu amempa, ni matumaini yangu kwamba haya tunayoanza kuyajenga sisi wafanyakazi tutayatumia vizuri, tutimize wajibu wetu na kila mmoja kwenye eneo lake aone umuhimu wa kuwa hapo alipo.”amesema Nape

Amesema Wizara hiyo inasimamia miradi mikubwa kadhaa ambayo itabadilisha na ni vizuri kama Wizara wakawa na uelewa wa pamoja wa miradi kupitia semina mbalimbali.

“Dunia inabadilika na sisi tuko kwenye Wizara ambayo inajenga kesho, mabadiliko ya sayansi na teknolojia, yanabadilisha namna ambavyo tunapaswa kufanya kazi hivyo ni muhimu kila mmoja kwenye eneo lake kuhakikisha anafkiria zaidi ya ‘google’ ili kuonesha umuhimu wa kuwa katika nafasi hiyo”amesema

Nae Katibu Mkuu Wizara ya Habari mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Jimmy Yonazi ameahidi kuboresha mazingira ya kazi kwa wafanyakazi.

“Jambo la kufanya kazi kwa furaha kwangu mimi ni kipaumbele, wajibu na nia, kila mmoja anatakiwa kufanya kazi kwa uhuru na kuruhusiwa kufikiri kwa sababu kufikiri kwa uhuru kunaleta ubunifu,

“Katika ulimwengu wa sasa, uchumi wa kidijitali hauna mipaka, vivyo hivyo kwa habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari havina mipaka kwa hiyo, tunamshkuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuamua kuunda Wizara hii na kuifanya nchi yetu kuwa moja ya nchi ambazo zina Wizara mahususi katika sekta hizi.”Amesema Yonazi

Amesema Endapo kila mmoja akifanya kazi kwa bidii na akatumika vizuri katika nafasi yake, Wizara hiyo itakuwa ya mfano ambayo kila mtu atatamani kuhamia. 

Kwa upande wake muwakilishi wa TUGHE Laurencia Masigo amesisitiza umuhimu wa mafunzo kwa wafanyakazi ili kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia.

“TUGHE inaipongeza Wizara kwa kupata hati safi kwa mwaka huu, tunawapongeza kwa sababu huo ni mchakato mrefu kuanzia kuweka mikakati na kuifuatilia, kupata fedha na kusimamia kazi mpaka kuja kukaguliwa na Wakaguzi na kupata hati safi, hili ni jambo la kujivunia, 

“TUGHE inaomba Watumishi waendelee kupatiwa mafunzo ya muda mfupi na mrefu ili kuweza kuendana na hali halisi ya mabadiliko ya kidijitali”amesema Masigo

No comments:

Post a Comment