 |
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda (kulia) akizungumza na Mkuu wa Idara ya Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF) ofisi ya Tanzania Dkt. Daniel Baheta (Kushoto). Dkt.Baheta alimtembelea Waziri Mkenda ofisini kwake jijini Dodoma kujadiliana mambo mbalimbali yahusuyo mageuzi ya elimu nchini. Picha na Wizara ya Elimu |
 |
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda (katikati) akizungumza na Mkuu wa Idara ya Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto (UNICEF) ofisi ya Tanzania Dkt. Daniel Baheta (Kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Sekta ya Elimu UNESCO Tanzania Faith Shayo walipokutana katika ofisi za Wizara jijini Dodoma kujadiliana mambo mbalimbali kuhusu mageuzi ya elimu nchini.Picha na Wizara ya Elimu |
Na Mwandishi wetu Dodoma
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda (Mb) leo Mei 6, Jijini Dodoma amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Idara ya Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa ya kuhudumia watoto (UNICEF) Ofisi ya Tanzania Dkt. Daniel Baheta na Mkuu wa Sekta ya Elimu UNESCO kwa upande wa Tanzania Faith Shayo.
Katika mazungumzo yao wamejikita katika masuala mbalimbali yanayohusu elimu hasa kuelekea Mkutano wa Kimataifa wa Elimu utakaofanyika mwezi Septemba 2022 nchini Marekani wenye lengo la kuleta mabadiliko Chanya katika Sekta ya Elimu.
Aidha,katika kikao hicho Waziri Mkenda amewahakikishia mashirika hayo ushirikiano katika kuleta mageuzi ya elimu nchini.
No comments:
Post a Comment