![]() |
Baadhi ya Washiriki katika ufunguzi wa Mafunzo kwa viongozi wa Shirikisho la Umoja wa Machinga yaliyofanyika jijini Dodoma leo tarehe 16/06/2022 |
Na WMJJWM,Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan awaahidi Viongozi wa Shirikisho la Machinga Milioni 10 kwa kila Mkoa ili kutatua changamoto na kero zao hapa nchini.
Rais Samia ameyasema hayo Mei 06,2022 jijini Dodoma wakati alipopiga simu katika ufunguzi wa mafunzo ya Viongozi wa Machinga kutoka Mikoa ya Tanzania Bara.
Ameongeza kuwa katika Mwaka wa fedha ujao wa 2022/23 Serikali itatoa fedha hizo kwa Kila Mkoa kwa Shirikisho la Umoja wa Machinga ili kutatua changamoto za uendeshaji wa Ofisi za Machinga zilizopo katika kila Mkoa.
“Nimesikia changamoto za uendeshaji wa ofisi na nina ahidi kutoa milioni kumi kwa kila mkoa ili kutatua kero hiyo” alisema Rais Samia
Akifungua mafunzo hayo Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima awapa Machinga mbinu mpya za kisasa ili waweze kupata matokeo chanya ambayo yataleta maendeleo ya Machinga na Taifa kwa jumla.
“Mheshimu uongozi wenu kwa ngazi za Wilaya na Mkoa ili mambo yaende sawa,utaratibu ufuatwe ili changamoto zenu ziweze kufanyiwa kazi kwa uharaka zaidi “alisema Dkt. Gwajima.
Aidha amewataka Machinga kufuata kanuni zilizowekwa ili kuhakikisha wanafanya biashara zao kwa amani bila kubuguziwa na vyombo vya usalama katika maeneo yao.
“Mtu mwenye kitambulisho chake anae fanya biashara zake na aheshimiwe na asifanyiwe fujo na vyombo vya usalama tutatembea kwa heshima kwani Rais ametuheshimisha”alisema Dkt. Gwajima.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Hamis amesisitiza Wamachinga wote bchini kwenda sambamba na jitihada za Serikali ili kuleta maendeleo chanya.
“Mhe.Rais amewatengenezea mazingira rafiki kwa kutatua changamoto zenu hivo basi tuhakikishe tunapata maendeleo kwa taifa letu” alisema Naibu Waziri Mwanaidi
Kwa upande wake Naibu katibu Mkuu wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Joseph Mwanakijij ameipongeza Serikali kwa kuliweka kundi hilo chini Wizara ya Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum ambayo imejikita katika kuwataftia fursa mbalimbali hapa nchini.
“Baada ya kutambulika Nchini jitihada mbalimbali zimefanyika kuhakikisha umoja huo unafika katika ngazi ya kitaifa na kutoa mafunzo mbalimbali ili kuwasaidia kuweza kufanikisha shughuli zao”amesema
No comments:
Post a Comment