Kamati ya Bunge yaipongeza Wizara ya Afya Huduma za VVU na UKIMWI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, August 27, 2022

Kamati ya Bunge yaipongeza Wizara ya Afya Huduma za VVU na UKIMWI


Kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala UKIMWI imeipongeza Wizara ya Afya kwa mafanikio makubwa katika kutekeleza afua za VVU na UKIMWI nchini.

Mwenyekiti wa Kama hiyo, Mhe. Fatma Taufiq (Mb) amesema hayo akiwaongoza wajumbe wa kamati kujadili na kupokea taarifa ya utekelezaji wa afua za VVU na UKIMWI iliyowasilishwa na wataalamu wa Wizara ya Afya - Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI wakiongozwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel (Mb) jijini Dodoma, tarehe 26.8.2022.

Mh. Taufiq amesema, kamati imefurahishwa na mafanikio katika afua zote ikiwemo upimaji wa VVU, Utoaji wa ARV, Uelimishaji, Manunuzi na usambazaji wa vitendanishi na kondomu na ukusanyaji wa takwimu za mwenendo wa VVU na UKIMWI.

Moja ya Majukumu ya Kamati ya kudumu ya Bunge Masuala UKIMWI ni kufuatilia utekelezaji wa sera na mipango ya Serikali kuhusu UKIMWI na udhibiti wake.

No comments:

Post a Comment