Asila Twaha, OR -TAMISEMI
Wadau wamaendeleo wametakiwa kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania ili kufanikisha Sekta ya Afya kufikia malengo katika kuboresha huduma za Afya nchini.
Rai hiyo imetolewa leo Jijini Dodoma na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Prof. Riziki Shemdoe katika hafla ya kupokea gari kutoka Shirika la Maendeleo ya Watu wa Marekani (USAID) kwa lengo la kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Akizungumza Prof. Shemdoe amesema Serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu utoaji huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi, kuimarisha mifumo ya shughuli za Ustawi wa Jamii na Lishe na kuwezesha kaya masikini kwa kuwajengea uwezo ili waweze kujitegemea katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Kwa upande wake mwakilishi kutoka Shirika la Maendeleo ya Watu wa Marekani(USAID) Dkt. Ify Udo ameishukuru Serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI ambao ndio wenye jukumu la kuwatambua watoto hao kuanzia ngazi ya mitaa kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa kuwasaidia hasa wanaoishi na VVU.
“lengo ni kuona watoto hawa wanapatiwa haki kama ilivyo kwa watoto wengine ili kufikia malengo ya Serikali” ameeleza Dkt. Udo


No comments:
Post a Comment