PROF.MKENDA ATANGAZA NEEMA KWA WANAFUNZI WENYE UFAULU WA JUU KATIKA MASOMO YA SAYANSI KIDATO CHA SITA 2022 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, September 27, 2022

PROF.MKENDA ATANGAZA NEEMA KWA WANAFUNZI WENYE UFAULU WA JUU KATIKA MASOMO YA SAYANSI KIDATO CHA SITA 2022

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda Akitoa tangazo rasmi linalohusu program mpya ya ufadhili wa SAMIA SCHOLARSHIP itakayotolewa kwa wanafunzi wenye ufaulu wa juu kwenye mitihani ya kidato cha sita mwaka 2022 iliyoendeshwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) katika taasusi za sayansi mbele ya Wadau wa elimu na waandishi wa habari leo Septemba 27,2022 jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Ali Abdugulam Hussein akizungumza wakati wa utoaji wa tangazo rasmi linalohusu program mpya ya ufadhili wa SAMIA SCHOLARSHIP itakayotolewa kwa wanafunzi wenye ufaulu wa juu kwenye mitihani ya kidato cha sita mwaka 2022 iliyoendeshwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) katika taasusi za sayansi mbele ya Wadau wa elimu na waandishi wa habari leo Septemba 27,2022 jijini Dodoma

Na Okuly Julius-Dodoma

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetoa tangazo rasmi linalohusu ufadhili wa SAMIA SCHOLARSHIP itakayotolewa kwa wanafunzi wenye ufaulu wa juu kwenye mitihani ya kidato cha sita mwaka 2022 iliyoendeshwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) katika taasusi za sayansi.

Akitoa Tangazo hilo leo Septemba 27,2022 jijini Dodoma Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema kuwa SAMIA SCHOLARSHIP ni ufadhili wenye thamani ya bilioni 3 ambapo itagharamia kwa asilimia (100%) masomo ya chuo Kikuu kwa wanafunzi hao ambao wamepata udahili katika fani za Teknojia,Uhandisi,Hisabati na Tiba.

"Mwanafunzi awe amepata udahili katika programu za Sayansi, teknolojia, uhandisi, Hisabati au tiba katika chuo kikuu hapa nchini kinachotambuliwa na Serikali ambazo zimetajwakatika kundi la kwanza (Cluster) katika mwongozo wa utoaji mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka 2022/2023 na awe ameomba ufadhili kwa usahihi kwa njia iliyoelekezwa,"Amesema Prof.Mkenda

Prof.Mkenda amesema kuwa Ufadhili huo utazingatia viwango na miongozo ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kugharamia maeneo yafuatayo ambapo ni Ada ya MafunzoPosho ya chakula na malaziPosho ya Vitabu na ViandikwaMahitaji Maalum ya VitivoMafunzo kwa Vitendo UtafitiVifaa saidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumuBima ya Afya na Wanafunzi watakaofadhiliwa, watagharamiwa kati ya miaka mitatu (03) hadi mitano (05) kulingana na programu husika walizodahiliwa.

Ambapo Maombi ya Samia Scholarship yatawasilishwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa njia ya mtandao https://olas.heslb.go.tz kwa siku 14 kuanzia Septemba 28, 2022.

Prof.Mkenda ameongeza kuwa Ufadhili huu ni wa asilimia mia moja ambao kikomo chake kitazingatia miongozo ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.Orodha ya majina ya wanafunzi husika inapatikana kupitia www.moe.go.tz na www.heslb.go.tz Alama za ufaulu: 3-5 (ME), 3-6 (KE) na 5-9 (wenye mahitaji maalum)

Kwa upande wake Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Ali Abdugulam Hussein amesema kuwa ufadhili huo utaongeza chachu kwa wanafunzi wengi kusoma masomo ya Sayansi,Teknolojia, uhandisi,Hisabati na Tiba.

"Idadi iliyopo mwaka huu naamini mwakani itaongezeka sana hivyo Mhe.Mkenda kama utaweza kuongea na Mhe.Rais tena aongeze walau Bilion zingine 3 kwa mwakani ziwe 6 kwa sababu naamini idadi itaongezeka maradufu kutokana na hamasa hii,"Amesema Mhe.Ali Abdugulam Hussein

UCHAMBUZI WA WANUFAIKA 640 wa SAMIA SCHOLARSHIP

Uwiano wa kijinsia wa wanufaika 640 wa Samia Scholarship ni; Wasichana 244 na asilimia 38% na Wavulana ni 396 sawa na asilimia 62%.Wanafunzi kutoka shule za serikali ni 396 sawa na asilimia 62% wakati Wanafunzi kutoka shule za binafsi ni 244 sawa na asilimia 38%.

Wanafunzi wenye ufaulu wa juu kiwango cha Alama tatu (3) ni 60 (9%)Wanafunzi kutoka shule za Tanzania Visiwani ni 43 (7%)Wanafunzi kutoka shule za Tanzania Bara 597 (93%)

Aidha jumla ya wanafunzi 11 wenye mahitaji maalumu watanufaika na Samia Scholarship.Hawa ni asilimia 100 ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu waliopata darala la kwanza katika tahasusi zinazolengwa na Samia Scholarship mwaka 2022/23

Shule zilizotia fora kwa kuwa na idadi kubwa za wanufaika wa Samia Scholarship ni pamoja na:Tabora Boys wanafunzi 79 (12%)St.Mary’s Mazinde Juu wanafunzi 51 (8%)Mzumbe Sekondari wanafunzi 46 (7%)Tabora Girls 39 (6%)Kisimili wanafunzi 31 (5%)

No comments:

Post a Comment