SERIKALI KUENDELEA KUIMARISHA HUDUMA ZA UMEME VIJIJINI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, September 3, 2022

SERIKALI KUENDELEA KUIMARISHA HUDUMA ZA UMEME VIJIJINI.


Na Mwandishi wetu Dodoma 

Serikali imeendelea na mikakati mbalimbali ili kuhakikisha utekeleza wa Miradi ya kusambaza umeme Vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato wakati wa kikao cha kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti kilichofanyika Bungeni Jijini dodoma,

Aidha, kamati ya Bunge ilijulishwa kuwa majadiliano ya mikataba 39, iliyowahusisha wakandarasi wa mradi wa kusambaza umeme Vijijini (REA), awamu ya III mzunguko wa II, utekelezaji wake unaendelea kwa kuwa majadiliano hayakuwa yamewasilisha utekelezaji wa Miradi.

Pamoja na mambo mengine, kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti ilitaka kujua bei ya kuunganishia wateja wapya waliopo maeneo ya Vijijini kutofautiana.

Hata hivyo, Byabato alisema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Nishati imekwishaunda timu ya wataalam ambayo iko kazini ili kuona uhalisia na hatimaye kuja na bei inayoendana na mazingira ya wananchi waishio katika maeneo ya Vijijini.

Vilevile wajumbe wa kamati ya Bunge, waliipongeza Taasisi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kazi nzuri inayotekelezwa na Wakala hiyo na kuitaka kuwa inatoa taarifa kwa wakati ili kuwezesha Wananchi kupata taarifa.

Pia kikao hicho, kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mha.Felchesmi Mramba, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mha.Hassan Seif Saidy, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Renata Ndege na Wataalam mbambali kutoka Wizara ya Nishati pamoja na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO).

No comments:

Post a Comment