NI 61,741,120 NDIO IDADI YA WATANZANIA -MHE.RAIS SAMIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, October 31, 2022

NI 61,741,120 NDIO IDADI YA WATANZANIA -MHE.RAIS SAMIA

Rais Samia akihutubia wakati akitangaza matokeo hayo ya Sensa leo Oktoba 31,2022 Jijini Dodoma
Rais Samia Suluhu Hassan akionesha kitabu cha matokeo ya mwanzo ya Sensa na Makazi mara baada ya kutangaza matokeo hayo kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo Oktoba 31, 2022. Kushoto ni Rais wa Zanzibar, Dkt Hussein Ali Mwinyi.
Rais Samia akizindua kitabu cha muongozo wa matumizi ya takwimu ya Sensa na Makazi.
Rais Samia akimkabidhi Rais wa Zanzibar, Dkt Hussein Ali Mwinyi kitabu cha matokeo ya mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi baada kuzinduliwa. Zanzibar hivi sasa ina zaidi ya wakazi mil. 1.8.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt Albina Chuwa akielezea kuhusu mafanikio ya sensa hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule akisoma taarifa ya mkoa huo na kutoa shukrani kwa Rais Samia kuupa mkoa huo heshima ya kutangazia matokeo hayo ya sensa.
Sehemu ya wananchi waliofurika kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kushudia Rais Samia akitangaza matokeo hayo.

Na Okuly Julius-Dodoma 

Hatimaye Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua matokeo ya mwanzo ya sensa ya watu na makazi na kutangaza kuwa Tanzania ina jumla ya watu Milioni sitini na moja laki saba na elfu arobaini na moja na mia moja ishirini (61,741, 120).

Rais Samia ametangaza idadi hiyo ya watu leo Katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma, ambapo amesema kuwa kati ya Idadi hiyo ya watu Tanzania Bara ni watu 59,851,357 na Zanzibar ni watu 1,889,773.

Amefafanua kuwa kati ya idadi hiyo ya watu Wanawake ni Milion 31,688790 sawa na asilimia 51 na wanaume ni milioni 30,53130 sawa na asilimia 49

Mhe.Rais Samia Ameeleza kuwa idadi hiyo ni Ongezeko la watu zaidi ya milioni 19 ukilinganisha na sensa ya miaka kumi iliyopita yaani 2012 ambapo kipindi hicho idadi ilikuwa milioni 44,928,923.

Pamoja na hayo Mhe.Rais Samia ametaja Mikoa iliyoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu ni Mkoa wa kwanza ni Dar-es-salaam ina watu milioni 5,383,728 na Mwanza ina watu milioni 3,699,872 hii ni kwa upande wa Tanzania Bara.

Na kwa upande wa Zanzibar Mkoa unaoongoza ni Mjini Magharibi yenye idadi ya watu zaidi ya laki nane

Rais Samia amewaagiza viongozi katika ngazi zote kutumia muongozo aliyouzindua leo kwa ajili ya kuzidi kuwaletea maendeleo watanzania.

"Ni wajibu wa kila mdau kuanzia sekta binafsi na sekta za umma kutumia muongozo huu kuwahudumia wananchi kwa sababu tayari tuna idadi ya watu tunaotakiwa kuwahudumia katika kila nyanja iwe ni huduma ya Afya,elimu na kwinginepo,"Amesema Mhe.Rais


No comments:

Post a Comment