KANZIDATA YA TAIFA YA UWEZESHAJI NI DARAJA TOSHA LA KUFANIKIWA KIBIASHARA-NEEC - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, November 8, 2022

KANZIDATA YA TAIFA YA UWEZESHAJI NI DARAJA TOSHA LA KUFANIKIWA KIBIASHARA-NEEC

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Beng'i Issa ,akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 8,2022 Jijini Dodoma kuhusu umuhimu wa Wafanyabiashara,Wawekezaji, watoa huduma ,mifuko ya Uwezeshaji na vikundi mbalimbali kujiunga na Kanzidata ya taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.
Meneja wa Tehama na Takwimu wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Isaac Dirangw,akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 8,2022 Jijini Dodoma kuhusu umuhimu wa Wafanyabiashara,Wawekezaji, watoa huduma ,mifuko ya Uwezeshaji na vikundi mbalimbali kujiunga na Kanzidata ya taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Beng'i Issa (kushoto) pamoja na Meneja wa Tehama na Takwimu wa Baraza hilo Isaac Dirangw (kulia) wakati wa mkutano wao na waandishi wa Habari leo Novemba 8,2022 jijini Dodoma.

Na Okuly Julius-Dodoma

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) , imetoa wito kwa Wananchi hasa wafanyabiashara wadogo na wakubwa kujisajili katika mfumo wa Kanzidata ya Taifa ya Uwezeshaji, ili kuunganishwa na wawekezaji katika sekta mbalimbali za uchumi na hasa katika uwekezaji mkubwa unaofanywa na Makampuni za nje hapa nchini.

Wito huo umetolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Beng'i Issa wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 8,2022 Jijini Dodoma kuhusu umuhimu wa Wafanyabiashara,Wawekezaji, watoa huduma ,mifuko ya Uwezeshaji na vikundi mbalimbali kujiunga na Kanzidata ya taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.

"Lengo kuu ni kuwaunganisha Wawekezaji na wafanyabiashara huku utafiti ukionesha kuwa kuna pengo kati ya makundi haya mawili, niseme tu hili ni jukwaa tosha la kuwakutanisha haya makundi na Asasi za kifedha ,mifuko ya uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya kijamii hivyo naamini watakopesheka,"

Na kuongeza kuwa "Pengo la kwanza ni kutojulikana nani ana nini na nani anahitaji nini na yuko wapi," Amesema Beng'i

Beng'i ameongeza kuwa Kanzidata hiyo itaisaidia Serikali kuratibu manunuzi ya ndani na kutoa fursa kwa makampuni zinazowekeza kufahamu bidhaa zinazopatikana kutoka kwa wafanyabiashara wa ndani.

Katibu Mtendaji huyo amesema kuwa katika Kanzidata pia baadhi ya wafanyabiashara hususani wadogo ambao hawana mitaji ya uhakika,hivyo itakuwa ni jukwaa la kuwafikia mifuko ya uwezeshaji ambayo inatoa mitaji kwa riba ndogo na masharti nafuu.

"Kanzidata hii haikuwasahau Mama lishe na Baba lishe ,Vikundi mbalimbali vya vijana ambao wanafanya shughuli ndogondogo za kiuchumi tunawashauri wajiunge kwenye vikundi vya pamoja za kiuchumi,kama wauzaji wa bidhaa za vyakula, wachomaji gril,watengeneza Samani mbalimbali za nyumbani na wenye ujuzi wowote ule wajisajili na hatimaye wajiunge na Kanzidata hii ili Watambulike,"Ameeleza Beng'i

Kwa upande wake Meneja wa Tehama na Takwimu wa Baraza hilo Isaac Dirangw , amesema moja ya faida kubwa ya kujiunga na Kanzidata hiyo ni kufanya bidhaa na huduma kuonekana na kujulikana na wadau mbalimbali wakiwemo Serikali, Wawekezaji na Wakandarasi.

"Mbali tu na bidhaa zako na huduma zako kwa ujumla kujulikana pia kuna fursa kubwa ya kupata mikataba na Makampuni makubwa na viwanda vikubwa , ikiwemo pia kujumuishwa katika mashindano makubwa ya kuwania tuzo katika Kongamano la kila Mwaka la Uwezeshaji Kiuchumi,"Amesema Dirangw

Kanzidata ya Taifa ya Uwezeshaji itawezesha Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, kupata taarifa, aina za shughuli za kiuchumi zinazofanyika na Taasisi au Mashirika na Mchango wao katika uwezeshaji wananchi kiuchumi hapa nchini.

Kanzidata ya Taifa ya Uwezeshaji inapatikana kupitia suppliers.uwezeshaji.go.tz

No comments:

Post a Comment