Na Okuly Julius-Dodoma
Hayo ameyasema leo Desemba 9,2022 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari akitangaza matokeo ya utafiti wa hali ya uzingatiaji maadili katika utumishi wa umma kwa mwaka 2022.
Waziri Mhagama amesema kuongezeka kwa matokeo hayo yanatokana na jitihada za kuimarisha uzingatiaji wa maadili chini ya Uongozi mahiri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
”Matokeo ya utafiti huu yanaonesha juhudi za serikali za kuchukua hatua mbalimbali za kuweka misingi imara ya usimamizi wa maadili, kuweka mazingira wezeshi na kuimarisha uwajibikaji katika utumishi wa umma.’amesema Waziri Mhagama
Aidha amemuagiza Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, kufanya kikao kazi cha pamoja na wadau kwa ajili ya kufanya majadiliano ya kina kuhusu matokeo ya utafiti huu na kuja na mikakati ya ufuatiliaji wa uzingatiaji wa maadili katika sekta zote kulingana na matokeo.
Pia amewataka Waajiri wahakikishe wanatenga bajeti ya mafunzo ya maadili na kuendesha mafunzo kwa watumishi wa umma walio kazini na wale wanaoajiriwa.
Waziri Mhagama Amesisitiza kuwa kuajiri wanaweka na kuimarisha mifumo ya utoaji wa mrejesho ndani ya taasisi zao ili kuendelea kutoa fursa kwa wananchi kukemea vitendo vya ukiukwaji wa Maadili.
No comments:
Post a Comment