******************
Na Okuly Julius-Dodoma
Imeelezwa kuwa mfumo wa ukusanyaji wa mapato Serikalini kwa njia ya mtandao(GePG) umeleta uoni mkubwa kwa serikali juu ya mapato yake na kupata takwimu sahihi ya makusanyo kwa urahisi.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao Mhandisi Benedict Ndomba wakati akielezea utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo mbele ya waandishi wa habari leo Februari 23,2023, Jijini Dodoma.
Ambapo Mhandisi Ndomba amesema kuwa Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na wizara ya fedha na mipango imetengeneza mfumo huo wa ukusanyaji wa mapato kwa lengo la kuimarisha uwazi na udhibiti katika ukusanyaji wa mapato ya serikali ambao kwa kiasi kikubwa umeleta matokeo chanya.
"mfumo huu wa ukusanyaji wa mapato Serikalini kwa njia ya mtandao(GePG) umeleta uoni mkubwa kwa serikali juu ya mapato yake na kupata takwimu sahihi ya makusanyo kwa urahisi na kweli umetengeneza uaminifu mkubwa pia kwa wananchi wanapofanya malipo yao kwani wamejua pesa zao zinakwenda moja kwa moja Serikalini,"amesema Mhandisi Ndomba
Aidha Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa Pamoja na kuongeza uoni kwa serikali mfumo huo umesaidia mapato ya serikali kuongezeka na kuiwezesha serikali kufanya mipango yake kwa usahihi.
Pia Mhandisi Ndomba ameongeza kuwa mfumo huo Umesaidia kuondoa ukwepaji wa malipo kwa baadhi ya taasisi ambazo zilikuwa hazilipi mapato kwa wakati.
"kwa sasa kila taasisi inalipa malipo yake kwa wakati na hakuna taasisi inayoweza kukwepa malipo yeyote kwani mfumo unasoma moja kwa moja pindi malipo yanapofanyika na pindi yanapochelewesha mfumo huo pia unajua,"amesema Mhandisi Ndomba
Mamlaka ya Serikali Mtandao ni matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika utendaji kazi wa Taasisi za Umma na utoaji wa huduma kwa wananchi na Lengo ilikiwa ni kuongeza ufanisi wa utendaji kazi katika Taasisiza Umma.


Safii
ReplyDelete