Na Okuly Julius-Dodoma
Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia imesema kuwa itaendelea kutengeneza mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia katika Vyuo vya Ualimu, kwa kuzingatia ujenzi bora wa majengo ,utunzaji wa mazingira na matumizi ya nishati mbadala.
Hayo yameelezwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof.James Mdoe leo Februari 23,2023, Mpwapwa , Mkoani Dodoma, wakati akifungua mafunzo ya siku nne ya utunzaji wa mazingira endelevu na ujanishaji kwa wakufunzi na menejimenti ya vyuo vya ualimu nchini ,yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu kupitia Mradi wa kuendeleza elimu ya ualimu (TESP).
Prof.Mdoe amesema kuwa serikali inatambua umuhimu wa mazingira na ndio maana imeweka mikakati mbalimbali ili kutunza mazingira ikiwemo kutumia nishati mbadala ya kupikia badala ya kutumia kuni na mkaa.
"Lengo la wizara ni kuweka alama katika lengo kuu la taifa la utunzaji wa mazingira endevu na ujanishaji kwa kuhakikisha mafunzo yanatolewa kwa walimu mpaka kwa wanafunzi yanajikita katika mbinu bora ya utunzaji ya mazingira hapo lengo la wizara litakuwa limetimia,''
Na kuongeza kuwa ''mafunzo haya yawasaidia kupunguza bajeti ya nishati na naamini baada ya ,afunzo haya mtakuwa mbele katika kupinga uharibifu wa mazingira,''amesema Prof.Mdoe
Kaimu Katibu Mkuu huyo amesema Mafunzo hayo ni muhimu kwa ujenzi wa taifa na wakufunzi ndio wajenzi wa taifa na hivyo ni vyema wakatumia mafunzo hayo kuleta tija katika vyuo vyao.
Hivyo ili kuleta tija ni vyema wakahama katika matumizi ya Mkaa,kuni kama nishati ya kupikia ili dhana ya utunzaji wa mazingira endelevu na ukijanishaji iweze kufikiwa.
"Kuhama kwenye matumizi ya kuni ni lazima tutahama na muweke pia kipaombele kwenya kuvuna maji ya mvua ili kuepuka matumizi holela ya maji,hiyo itawasaidia kupunguza matumizi na bajeti kubwa,''amesistiza Prof.Mdoe
Prof.Mdoe amewakumbusha Wakufunzi hao kuwa , ndio wamebeba ndoto ya vizazi vya sasa na vijavyo kwani wakiwafundisha walimu vizuri nao wakienda kuwafundisha wanafunzi vizuri itawasaidia kubadisha fikra yao juu ya utunzaji wa mazingira endelevu na ujanishaji.
"Lengo la wizara ni kuweka alama katika lengo kuu la taifa la utunzaji wa mazingira endevu na ujanishaji kwa kuhakikisha mafunzo yanatolewa kwa walimu mpaka wanafunzi hapo lengo la wizara litakuwa limetimia,"amesema Prof.Mdoe
Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi wa Elimu ya Ualimu kutoka Wizara ya elimu,sayansi na teknolojia Huruma Mageni amesema kuwa mafunzo hayo yatatolewa kwa vyuo vyote 35 hapa nchini amabapo mpaka sasa vyuo 14 tayari vimeshapatiwa mafunzo hayo.
"Mafunzo haya ya utunzaji wa mazingira endelevu na ujanishaji kwa wakufunzi na menejimenti ya vyuo vya ualimu nchini ni mahususi kabisa kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kuwajengea wakufunzi uelewa juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira kwa kutumia nishati mbadala na kupanda miti katika mazingira ya vyuo ila nao wakawafundishe walimu wanafunzi kwa ajili ya kufikisha kwa wanafunzi huko mashuleni,"amesema Mageni







No comments:
Post a Comment