Katika mchezo huo wa pili, Wananchi walipata mabao yao kupitia kwa Mshambuliaji Kennedy Musonda Mudathir Yahya Abbas na bao la tatu limefungwa na Winga wa Tuisila Kisinda kwenye dakika ya huku bao la TP Mazembe limefungwa na Alex Ngonga.
Yanga SC wameondoka na alama tatu muhimu sanjari na kiasi cha fedha Shilingi Milioni 15/- za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye aliahidi kiasi cha Shilingi Milioni 5/- kwa kila goli ambalo litafungwa na timu za Tanzania ambazo zinacheza Michuano ya Kimataifa, huku wakichukua Milioni 3/- za Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
Kundi D la Michuano hiyo ya CAF CC, US Monastir wanaongoza Kundi hilo wakiwa na alama nne wakati TP Mazembe licha ya kufungwa mchezo wa leo wana alama tatu sawa na Yanga SC wenye kama hizo huku Real Bamako wanaburuza mkia wakiwa na alama moja pekee.
Yanga SC watawacheza ugenini dhidi ya Real Bamako ya Mali mchezo unaofuata wakati TP Mazembe wakiwa na kazi dhidi ya US Monastir ya Tunisia.
No comments:
Post a Comment