Shujaa wa Simba SC ni Mshambuliaji hatari katika Michuano hiyo Jean Baleke alifunga dakika ya 30 na bao hilo liliwapeleka wenyeji Mapumziko wakiwa wanaongoza.
Kwa ushindi huo Simba SC wataenda nchini Morocco katika marudiano wakiwa na bao moja hivyo kwenda kutafuta bao jingine au sare ili waweze kutinga hatua ya Nusu Fainali Aprili 29 watarudiana tena.
Wawakilishi katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika timu ya Yanga SC watashuka dimbani kesho kucheza na Rivers United nchini Nigeria.
CHANZO NI MZALENDO BLOG
No comments:
Post a Comment