Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amefanikisha kufanyika kwa mchakato wa maboresho ya mfumo wa ununuzi wa Wakala Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kwa kushusha shughuli za ununuzi kwenye ngazi ya Mikoa tofauti na ilivyokuwa ambapo ununuzi ulikuwa unafanyika kwenye ngazi ya Makao Makuu pamoja na kwenye Kanda tisa.
Aidha, Maboresho hayo yaliyofanyika kwenye kikao cha Mhe. Waziri wa Maji na Menejimenti ya Wizara pamoja na Menejimenti ya RUWASA jijini Dodoma yamelenga kuongeza tija kwenye shughuli za ununuzi za Wakala, kuongeza kasi ya ununuzi, thamani ya Fedha za Umma na kutoa fursa kwa Wazabuni, Wakandarasi na Watoa huduma waliopo kwenye Mikoa yote ya Tanzania Bara ambalo ndio eneo la kiutendaji la RUWASA.
Katika hatua nyingine Aweso amesisitiza kuwa maboresho haya ni muhimu sana kwani yatarahisisha muda wa kufanyika kwa manunuzi pamoja na kwamba swala hili ni sehemu ya kuzingatia maoni ya waheshimiwa wabunge na wadau mbali mbali katika kuongeza tija kwenye shughuli za ununuzi na ugavi kwa Wakala. Sambamba na maboresho hayo.
Mwisho Mhe.Waziri ameiagiza Menejimenti ya Wizara kuifanyia kazi changamoto ya Maafisa ununuzi na ugavi ambayo ipo RUWASA kwa kuhakikisha wanaongezwa watumishi hao ili kuendana na mfumo mpya uliofanyika.
Mfumo huo unatarajiwa kuanza kutumika mwanzoni mwa mwaka wa fedha 2023/2024.
No comments:
Post a Comment