DKT. KIRUSWA: WIZARA KUENDELEA KUWAUNGANISHA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI NA TAASISI ZA FEDHA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, May 8, 2023

DKT. KIRUSWA: WIZARA KUENDELEA KUWAUNGANISHA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI NA TAASISI ZA FEDHA


Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa amesema Wizara imejipanga kuendelea kuwawezesha na taasisi za fedha wachimbaji wadogo wa madini ili wapatiwe mikopo kwa lengo la kuchimba kwa tija na kukua kutoka kwenye uchimbaji mdogo kwenda wa kati na hatimaye kwenda kwenye uchimbaji mkubwa.


Dkt. Kiruswa amesema hayo wakati akikagua mabanda ya maonyesho katika Kongamano la Mkutano Mkuu wa FEMATA linaloendelea jijini Mwanza ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele chake.


Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima amelipongeza Shirikisho la Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA) kwa maamuzi ya kufanya Kongamano la kwanza mkoani humo.


"Sisi kama mkoa wa Mwanza tunaipongeza FEMATA kwa maamuzi ya kuleta Kongamano hili jijini Mwanza, tunawahakikishia ulinzima na usalama katika kipindi chote mkiwa hapa mwanza," amesema Malima.


Naye, Rais wa FEMATA John Bina amesema zaidi ya mada 22 zimewasilishwa na wataalamu mbalimbali kwa wachimbaji wadogo wa madini katika Clinic ya Madini inayoendelea katika viwanja vya Rock City Mall Jijini Mwanza.

No comments:

Post a Comment