PROF.MKENDA:SHULE ZA SEKONDARI ZA UFUNDI KUFUFULIWA,KUANZA USAILI RASMI JANUARY 2024. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, May 12, 2023

PROF.MKENDA:SHULE ZA SEKONDARI ZA UFUNDI KUFUFULIWA,KUANZA USAILI RASMI JANUARY 2024.

Waziri Wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda,akizungumza wakati akifungua Kongamano la Sera na Mitaala ya Elimu kuhusu uhuishaji wa sera na Mitaala ya Elimu ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023,Leo Mei 12,2023 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo,akizungumza katika Kongamano la Sera na Mitaala ya Elimu kuhusu uhuishaji wa sera na Mitaala ya Elimu ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023,Leo Mei 12,2023 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu,Utamaduni na Michezo Profesa Kitila Mkumbo,akizungumza katika Kongamano la Sera na Mitaala ya Elimu kuhusu uhuishaji wa sera na Mitaala ya Elimu ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023,Leo Mei 12,2023 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma.

Na Okuly Julius-Dodoma

Waziri Wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda,amesema katika maboresho yanayofanyika sasa ya Sera ya Elimu na Mitaala,Serikali imedhamiriankufua shule za Sekondari za Ufundi zinazotarajiwa kuanza kuchukua wanafunzi kuanzia Januari mwakani.


Shule hizo ni pamoja na Moshi Tech, Ifunda Tech, Mtwara Tech, Tanga Tech, Chato Tech, Iyunga Tech, Musoma Tech, Bwiru Tech na Mwadui Tech


Mbali na hilo imesema ,imetoa mapendekezo ya namna nzuri ya kuajiri walimu wa kuanzia elimu ya awali,msingi,sekondari na vyuo vya ualimu hapa nchini.


Akifungua Kongamano la Sera na Mitaala ya Elimu kuhusu uhuishaji wa sera na Mitaala ya Elimu ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023,Waziri wa Elimu,Sayansi na Tekonolojia Prof. Adolf Mkenda amesema,mapendekezo ya kufufua shule za sekondari za ufundi ni kutokana na vijana wengi kuona kama kusoma ufundi bila kuwa na elimu ya sekondari ni kujidhalilisha .


“Tumetenga bajeti ya kurudisha shule zetu za sekondari za Ufundi,hii ni kwa sababu tumeona vijana wengi wakienda kusoma katika vyuo vya ufundi,wanarudi tena kufanya mtihani wa kidato cha sita ili waende vyuo vikuu.”alisema Prof.Mkenda



Aidha amesema,katika mapendekezo ya Sera mpya ya Elimu na Mitaala serikali imependekeza elimu ya msingi iwe kwa kipindi cha miaka 6 badala ya 7 lakini pia mwanafunzi lazima asome shule ya msingi na sekondari (O-Level).


Amesema Elimu ya Sekondari itakuwa na Mikondo amiwili ya Elimu ya Jumla na Elimu ya Amali (Ufundi na ufundi stadi ) ambapo katika elimu ya Amali wanafunzi watafundishwa ufundi kwa vitendo ambapo kila mkondo utakuwa na michepuo yake.



Akizungumza kuhusu namna ya kupata walimu Prof.Mkenda amewatoa wasiwasi walimu waliopo kazini huku akisema utaratibu huo hautawahusu.


“Niwatoe hofu walimu waliopo kazini,tutakapoanza utaratibu mpya wa kupata walimu ,wao hawatahusika na wataendelea na kazi mpaka watakapo staafu na badala yake Serikali itaangalia namna ya kuwapa nafasi ya kwenda kujiendeleza kielimu.”amesisitiza Mkenda


Alisema ,mapendekezo kuhusu utekelezaji wa sera hiyo utawekwa katika kalenda kwa ajili ya kuanza kutumika kwa majaribio Januari mwakani.



Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema,Katika utekelezaji wa rasimu hiyo kulikuwa na kamati mbili ambazo ni Kamati ya Mapitio ya Sera na Kamati ya Mabadiliko ya Mitaala ambazo Kila Moja imefanya kazi ya kukusanya maoni ambapo zaidi ya wadau 200,000 walifikiwa na kupata fursa ya kutoa maoni yao kuhusu maboresho ya sera na mitaala ya elimu hapa nchini .


“Sera hiyo na Mitaa haijaangalia tu wakati uliopita ili imechambua hali halisi iliyopo kwa sasa katika elimu yetu kuanzia elimu ya awali,msingi,sekonda mpaka elimu ya ualimu.”amesema Profesa Nombo



Awali Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu,Utamaduni na Michezo Profesa Kitila Mkumbo amesema,kongamano hilo ni fursa kwa wabunge kuchukua maoni na kuyafanyia kazi ili kuhakikisha serikali inayachukua lakini pia kwa yale ya kisheria,Kamati hiyo itahakikisha Sheria inatungwa .


“Kumekuwa na changamoto katika mfumo wetu wa Elimu,ndiyo maana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza ufanyiwe kazi kwa ajili ya kupata sera na mitaala bora itakayowezesha wahitimu kujiari na kuisaidia jamii na Taifa kwa ujumla.”amesisitiza Prof.Mkumbo

No comments:

Post a Comment