OR-TAMISEMI YAWEKA WAZI MAJINA YA WANAFUNZI WATAKAOJIUNGA KIDATO CHA TANO 2023. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, June 11, 2023

OR-TAMISEMI YAWEKA WAZI MAJINA YA WANAFUNZI WATAKAOJIUNGA KIDATO CHA TANO 2023.


Na Okuly Julius-Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Angellah Kariuki amesema Watahiniwa 192,348(36.95%) waliomaliza kidoto cha nne mwaka 2022 na kupata ufaulu wa Daraja la I –III wamechaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano katika Shule za Sekondari, Vyuo vya Ualimu, Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Kati vya Serikali Mwaka 2023.


Ambapo kati ya hao Tanzania Bara walikuwa na watahiniwa 188,128 wakiwemo wasichana 84,509 na wavulana 103,619.


Mhe.Kairuki ameyasema hayo Leo Juni 11,2023 Jijini Dodoma wakiti akitoa Taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari kuhusu kukamilika Kwa Zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa Kujiunga na Kidato cha Tano katika Shule za Sekondari, Vyuo vya Ualimu, Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Kativya Serikali Mwaka 2023.


"Zoezi hili limefanyika kwa kuzingatia takwimu za matokeo ya Wanafunzi waliofanya Mtihani wa Kidato cha Nne Mwaka,2022,kutoka Tanzania Bara," 


Na kuongeza kuwa "Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka Shule za Serikali, zisizo za Serikali, watahiniwa wa kujitegemea waliofanya mtihani chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi,"ameeleza Mhe.Kairuki


Mhe Kairuki amesema kuwa Wanafunzi wote waliopangwa kujiunga na Kidato cha Tano kwa mwaka,2023 wanapaswa kuanza kuripoti Shuleni kuanzia tarehe 13 Agosti,2023 na Siku ya mwisho ya kuripoti itakuwa tarehe 31 Agosti, 2023.


Mhe.Kairuki amesema Idadi hiyo inajumuisha pia Wanafunzi wenye Mahitaji Maalum 490 ambapo wasichana ni 218 na wavulana ni 272.


Ambapo Wanafunzi wote 188,128 waliokidhi vigezo wamechaguliwa na kupangiwa 
kujiunga na Kidato cha Tano katika shule mbalimbali nchini pamoja na Vyuo vya fani mbalimbali.


Wanafunzi 129,830 wakiwemo wasichana 66,343 na wavulana 63,487 sawa na asilimia 69 ya wenye sifa, wamechaguliwa kujiunga na Shule za Sekondari za Kidato cha Tano kwa mchanganuo ufuatao,


Wanafunzi 1,878 wakiwemo wasichana 1,097 na wavulana 781 wamepangiwa katika Shule za sekondari Maalum 8 za Kilakala, Mzumbe, Ilboru, Kisimiri,Msalato,Kibaha, Tabora Boys na Tabora Girls.


Huku wanafunzi 122,908 wakiwemo wasichana 62,731 na wavulana 60,177 wamepangiwa katika shule 519za Sekondari za Bweni za
Kitaifa za Kidato cha Tano.


Aidha, Mhe.Kairuki amesema Wanafunzi 5,044 wakiwemo wasichana 2,515na wavulana 2,529 wamepangwa katika Shule 11 za Sekondari za Kutwa za Kidato
cha Tano.


Pia amebainisha kuwa Wanafunzi 58,298 wakiwemo wasichana 18,166 na wavulana 40,132 sawa na asilimia 31 wamepangiwa kujiunga kwenye kozi mbalimbali za Stashahada katika Vyuo vya Kati vinavyosimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu yaUfundi (NACTVET.


MCHANGANUO KWA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KOZI MBALIMBALI KATIKA VYUO VYA KATI
 
Wanafunzi 1,645wakiwemo wasichana 646na wavulana 999 wamechaguliwa kujiunga na Vyuo vya Ualimu ngazi ya Stashahada ya
Sayansi, Hesabu na TEHAMA.


Wanafunzi 1,877 wakiwemo wasichana 757na wavulana 1,120 wamechaguliwa kujiunga na fani mbalimbali katika Vyuo 04vya Elimu ya Ufundi ambavyo ni Chuo cha Ufundi cha Arusha (ATC), Taasisi ya
Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo Kikuu cha Sayansi na
Teknolojia Mbeya -MUST na Chuo cha Usimamizi na Maendeleo ya
Maji (WDMI).
 

Wanafunzi 1,842 wakiwemo wasichana 943 na wavulana 899 wamechaguliwa kujiunga na fani mbalimbali katika Vyuo 04 vya Elimu ya Ufundi ambavyo ni Chuo cha Ufundi cha Arusha (ATC), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo Kikuu cha Sayansi na
Teknolojia Mbeya -MUST na Chuo cha Usimamizi na Maendeleo ya
Maji (WDMI).



Wanafunzi 52,934 wakiwemo wasichana 15,820 na wavulana 37,114wamechaguliwa kujiungakwenye kozi mbalimbali zikiwemo za Kilimo,Ufugaji,Utawala, Biasharana zinginezo za Stashahada katika Vyuo vya kati mbalimbali nchini.


Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, Vyuo vya
Ualimu na Vyuo vya Elimu ya Ufundi mwaka, 2023 inapatikana kwenye tovuti ya
Ofisi ya Rais -TAMISEMI ya selform.tamisemi.go.tz na Baraza la Taifa la Elimu ya
Mafunzo ya Ufundi ya www.nacte.go.tz.


Mhe.Kairuki amewataka wazazi ,walezi na wanafunzi watakaopata changamoto yeyote kutoa taarifa katika Ofisi za Halmashauri,Mikoa na ikiwezekana Ofisi ya Rais -TAMISEMI ili kuepusha mkwamo wowote utakaojitokeza.




No comments:

Post a Comment