OXYGEN : PROGRAMU YA KIJAMII YA MAWASILIANO ILIYOTENGENEZWA NA VIJANA WA KITANZANIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, June 7, 2023

OXYGEN : PROGRAMU YA KIJAMII YA MAWASILIANO ILIYOTENGENEZWA NA VIJANA WA KITANZANIA


Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) imetengeneza programu ya kijamii ya mawasiliano iitwayo Oxygen inayowezesha kufanya mawasiliano kwa njia ya mazungumzo, ujumbe mfupi (SMS), sauti, video, picha pamoja na aina mbalimbali za mafaili.

Programu hii inafanya kazi kama programu nyingine za kijamii na shirikishi zikiwemo WhatsApp, Telegram na Skype, huku programu ya Oxygen ikiwa na vitu vingi vya ziada.

Meneja wa Kituo cha Utafiti na Ubunifu na Uendelezaji wa Serikali Mtandao (eGovRIDC) kutoka Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Dr. Jaha Mvulla, alisema lengo la programu hiyo ni kuwezesha na kurahisisha mawasiliano baina ya familia, marafiki na timu zinazofanya kazi pamoja.

‘Programu ya Oxygen inaweza kutumika kwa soga za faragha na umma kwa kuwawezesha watumiaji kuwasiliana kwa njia ya sauti, video, jumbe fupi (SMS), picha na mafaili ‘ alifafanua Dr. Jaha.

Alieleza kuwa, Programu hii imetengezwa kwa ajili ya kusaidia watumiaji kuwasiliana kwa njia mbalimbali kwa kuzingatia usalama wa hali ya juu wa taarifa za watumiaji (end-to-end encryption).

‘Programu hii inaweza kutumiwa na mwananchi yeyote kinachohitajika ni mtumiaji kuwa na namba ya Simu pamoja na kifaa kinachoweza kutumika kama vile Simu janja (smartphone) au kompyuta kupitia kivinjari (browser)’ Alifafanua.

Programu ya Oxygen imetengenezwa na vijana wa kitanzania kupitia Kituo cha Utafiti na Ubunifu na Uendelezaji wa Serikali Mtandao (eGovRIDC) cha e-GA na imeshauriwa wananchi kutumia programu hii ili kuendeleza bunifu za ndani.

No comments:

Post a Comment