MEJA JENERALI MBUGE: TUTUMIE RASILIMALI ZILIZOPO KUKABILI MAAFA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, July 3, 2023

MEJA JENERALI MBUGE: TUTUMIE RASILIMALI ZILIZOPO KUKABILI MAAFA

Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Meja Jenerali Charles Mbuge akimsikiliza Mratibu wa maafa wa ofisi yake Bi.Numpe Mwambenja alipotembelea banda la Ofisi hiyo katika maonesho ya Kimataifa ya Biashara maarufu Sabasaba yanayoendelea ndani ya viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 3 Julai, 2023.
Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri MMkuu Sera, Bunge na Uratibu Meja Jenerali Charles Mbuge akizungumza na watendaji wa idara yake alipowatembelea katika banda la ofisi hiyo kwenye maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali wakiwa katika Banda la Idara ya Menejimenti ya maafa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) katika maonesho ya Kimataifa ya Biashara maarufu Sabasaba yanayoendelea ndani ya viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Maafa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Khowe Malegeri akitoa maelezo kuhusu masuala ya menejimenti ya maafa katika maonesho ya sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri MMkuu Sera, Bunge na Uratibu Meja Jenerali Charles Mbuge akiuliza jambo kuhusu masuala ya afya za polisi alipotembelea banda la Jeshi la Polisi Tanzania Kikosi cha Afya katika maonesho ya Sabasaba
Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Meja Jenerali Charles Mbuge akiangalia moja ya kiatu katika banda la Jeshi la Polisi kikosi cha Polisi Ufundi alipotembelea banda hilo katika maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Maafa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Numpe Mwambenja akitoa maelezo kwa wadau waliotembelea banda la ofisi hiyo katika maonesho ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba.
Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri MMkuu Sera, Bunge na Uratibu Meja Jenerali Charles Mbuge akifurahia Muziki wa Bendi ya Polisi alipotembelea banda la Jeshi la Polisi katika maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri MMkuu Sera, Bunge na Uratibu Meja Jenerali Charles Mbuge akizungumza jambo kuhusu zao la bangi alipotembelea banda la Jeshi la Polisi katika maonesho ya Sabasaba yanayoendelea Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali wakiwa katika Banda la Idara ya Menejimenti ya maafa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) katika maonesho ya Kimataifa ya Biashara maarufu Sabasaba yanayoendelea ndani ya viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)


NA. MWANDISHI WETU

Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Meja Jenerali Charles Mbuge ameiasa jamii kuendelea kutumia rasilimali zilizopo katika masuala ya menejimenti ya maafa nchini.


Ametoa kauli hiyo alipotembelea na kujionesha shughuli zinazoendelea katika banda la Ofisi yake katika maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.


Meja Jenerali Mbuge alisema kuwa ni muhimu kuendelea kujiandaa na kujilinda na maafa kwa kutumia rasilimali zilipo nchini ili kuwa na mazingira salama na bora katika nchi yetu.


“Tutumia rasilimali tulizonazo katika masuala haya ya maafa kwa kuzingatia masuala ya usimamizi wa maafa ni jukumu la kila mmoja katika eneo lake huku tukizingatia maelekezo ya kitaalam ya usimamizi wa maafa nchini,”alisema


Aidha alitumia fursa hiyo kuikumbusha jamii kuendelea kufuatilia taarifa za hali ya majanga na tahadhali zinazotolewa na Mamlaka husika ili kuwa na utaratibu wa kujiandaa, kuzuia, kukabili na kurejesha hali pindi maafa yanapotokea.

No comments:

Post a Comment